LATEST POSTS

Saturday, May 3, 2014

MAJONZI CHUO KIKUU MZUMBE WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA WAFA WAKIOGELEA MTONI....




katibu Mkuu Kanisa la Uinjilist Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Msemaji wa Kanisa hilo Jacobo Mwakasole  akizungumzia namna tukio la vifo vya wanafunzi hao vilivyo tokea katika eneo hilo la kuhifadhia wanyama pori Zoo ya Ifisi Mbaralizi mbalizi  na hiyoo ndo boti iliouwaa wanafunzi   
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe Campus ya Mbeya Prof.Ernest Kihanga akitoa maelezo juu ya vifo vya wanafunzi hao



WANAFUNZI wawili wa Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, wamepoteza maisha baada ya kuzama kwenye bwawa la maji la kunyweshea wanyama lililopo kwenye hifadhi ndogo ya Bonde la Ifisi Wilayani Mbeya.

Bwawa hilo linamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Uinjilist lililopo eneo la  Mbalizi, limetengenezwa kwa ajili ya matumizi maalum ya kuhifadhi maji ili kutumika nyakati za kiangazi kwa ajili ya wanyama ambao wamehifadhiwa kwenye bonde hilo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiutalii.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe Campus ya Mbeya, Profesa Ernest Kihanga, amesema uongozi ulipata taarifa majira ya saa kumi jioni ya kwamba wanafunzi wawili ambao ni Maiko Tarime na Albart Shenkalwa wote wamezaliwa katika  miaka ya 1991 na 1992.

Amesema, Marehemu Maiko anaishi Mkoani Tabora huku marehemu Albart ni mkazi wa Tanga ambao wote kwa pamoja wanatarajiwa kusafirishwa leo(jana) kuelekea nyumbani kwao kwa ajili ya maziko.

Akielezea tukio hilo, Kihanga amesema wanafunzi hao ambao inasemekana walikuwa 14 wanaume kwa wanawake waliongozana kwa pamoja na kwenda kwenye hifadhi hiyo kwa ajili ya kuangalia wanyama mara baada ya chuo hicho kufungwa kwa muda wa wiki moja.

Amesema, imeelezwa kwamba baada ya wanafunzi hao kuingia kwenye bwawa hilo la maji wakitumia Mitumbwi na Boti zilizokuwa pembeni ndipo boti ilipinduka na marehemu Maiko kuanza kuzama.

Kwa upande wake Waziri Mkuu serikali ya wanafunzi, Warioba Marato, alisema kuwa wanafunzi wamepokea taarifa ya msiba kwa mshtuko na kwamba wameushukuru uongozi wa chuo hicho kwa kutoa ushirikiano kuanzia tukio lilipotokea hadi hatua ya mwisho ya kuhakikisha miili hiyo ikisafirishwa nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Naye Katibu Mkuu wa kanisa la Uinjilist  Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole, alisema kuwa  wanafunzi hao wakiwa na wenzao wakike wapatao 14 walifika kwenye kituo hicho kwa ajili ya kutembelea wanyama mbalimbali ambao wemehifadhiwa kwenye hifadhi hiyo.
Amesema, wakati wanafunzi hao wakitembezwa na muhusika wa kituo walifika kwenye bwawa hilo la maji na kutaka kuingia ndani ya maji kitendo ambacho kilizuiliwa na mmoja wa watumishi kwenye hifadhi hiyo.

Amesema, Kwa mujibu wa msimamaizi huyo wa kituoa, wanafunzi hao walikuwa ni wabishi hivyo wanafunzi wawili waliingia ndani ya Boti huku wanafunzi zaidi ya nane wakipanda mtumbwi ikiwa ni kinyume cha utaratibu huku wakicheza na kurusha maji ovyo.

Amesema, Boti hiyo ilipinduka ndipo marehemu Maiko alipozama na marehemu
Albart  alipomuona mwenzake anazama ndipo alipoingia ndani ya maji kwa ajili ya kumuokoa ambapo jitihada hizo ziligonga mwamba na wote wawili wakijikuta wakipoteza maisha.

Aidha, uongozi wa Kanisa hilo umesikitishwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa hifadhi hiyo ndogo na kwamba limetoa pole kwa ndugu na jamaa waliondokewa na ndugu zao.

Hata hivyo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msani alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa uongozi wa Chuo kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Mwisho

0 comments: