KESI dhidi ya maafisa
wazamani wa serikali ya Malawi wanaodaiwa kuhusika na wizi wa mamilioni
ya dola za Marekani kutoka hazina ya serikali inatarajiwa kuanza kesho.
Sakata
hilo lilifichuliwa kufuatia jaribio la mauaji dhidi ya Mkurugenzi wa
bajeti, Paul Mphwiyo, ambaye ameripotiwa alikuwa tayari kufichua kashfa
kubwa zaidi .
Kwa mujibu wa BBC, inaelezwa kwamba hiyo ni kashfa kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Malawi.
Kashfa
hiyo inayojulikana kama Cashgate imevuruga uhusiano mzuri ulioko kati
ya Malawi na wafadhili huku raia wakikasirishwa na wizi huo wa mali ya
umma.
Kashfa hiyo inaanzia katika eneo la kompyuta ambapo habari za siri kuhusu uwekaji fedha zimehifadhiwa.
Maafisa
kadhaa wa Serikali wa mekuwa wakitumia udhaifu fulani katika mpango wa
uhifadhi wa kompyuta hizo na kuiba mamilioni ya pesa kutoka hazina ya
Serikali.
Inadaiwa kwamba huenda dola milioni 250 za Marekani
ziliporwa kwa kuwalipa wafanyabiashara kimagendo kwa huduma ambazo
hazikutolewa kwa Serikali.
Habari za uporaji huo wa mali ya umma
zilifichuka wakati Mkurugenzi wa Bajeti katika Wizara ya Fedha, Paul
Mphwiyo, alipopigwa risasi Septemba mwaka 2013.
Tukio hilo
lilitekelezwa siku chache kabla ya mfanyakazi wa cheo cha chini
serikalini alipopatikana na pesa taslimu ya dola 300,000 za Marekani
katika buti la gari lake.
Pesa nyingi zaidi zilipatikana na kupokonywa wafanyakazi wa umma majumbani mwao katika buti za magari yao..
0 comments:
Post a Comment