LATEST POSTS

Sunday, January 19, 2014

Mama wa kambo amlisha kinyesi mtoto

MWANAMKE mmoja amekamatwa na raia wema katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, na kufikishwa katika kituo cha polisi baada ya kudaiwa kumnyanyasa mtoto wa kambo wa miaka minne, kwa kumpiga na kumlisha kinyesi chake kwa madai ya kujisaidia ndani ya nyumba yake.
Joyce Maneno, mkazi wa mtaa wa Idara ya maji katika mji huo, alikamatwa na wananchi wa eneo hilo, baada ya kugundua kunyanyaswa kwa mtoto huyo ambaye umchapa, umpiga, na kumlisha kinyesi chake.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Bunda, Chiku Mshora, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa liliripotiwa polisi na mwanamke huyo alikamatwa.
Alisema kuwa baada ya muda mwanamke huyo alidhaminiwa na kutoka huku akidaiwa kujigamba kuwa atafanya jambo lolote baya zaidi dhidi ya mtoto huyo.
“Baada ya mwanamke huyo kudhaminiwa polisi, alisikika akijigamba kuwa mtoto huyo atamfanyia jambo lolote lile, kwani hawezi kumwaribia maisha yake kwa mumewe,” alidai Mshora.
Baadhi ya mashuhuda walidai kusikia kilio kinachotokana na kipigo kutokana kwa mtoto huyo hata wakati mwingine mwanamke huyo humtoa nje kutokana na kudai kujisaidia haja kubwa ndani ya nyumba.
“Sisi tuligundua baada ya kila siku kusikia mtoto analia kwa kipigo, tena alikuwa akichovya fimbo aliyompigia katika kinyesi na kumlisha,” alidai mmoja wa mashuhuda.
Walisema kuwa kutokana na udogo wa mtoto huyo, anashindwa kufungua mlango hatua inayomlazimu kuenda haja kubwa ndani ya nyumba.
Wananchi hao walidai kuwa mwanamke huyo ufanya ukatili huo mara kwa mara, hasa pale mume wake anapokuwa visiwani kwenye shughuli zake za uvuvi.
Wakati huo huo, mtoto mdogo aliyeozwa kwa mwanaume wa miaka 54, amepelekwa kwenye kituo cha kulea watoto kiitwacho Jipe Moyo, kilichoko mjini Musoma, ili aweze kutunzwa huko na kusomeshwa.
Mtoto huyo aliolewa na mwanamume huyo baada ya kutoa kishika uchumba kiasi cha sh 55,000 kwa baba mzazi wa mtoto huyo, ambapo hivi sasa wazee hao  wapo mahabusu kutokana na kukosa dhamana.
 
Chanzo: Tanzania

0 comments: