MKUU wa Wilaya (DC) ya
Igunga, Elibariki Kingu, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwafukuza
kazi watumishi wawili wa zahanati ya Kijiji cha Isakamaliwa kwa kudharau
maelekezo yake ya kuwataka warudi sehemu yao ya kazi.
Watumishi wa halmashauri
wanaotakiwa kufukuzwa kwa kukaidi agizo la mkuu wa wilaya ni Daktari wa
zahanati, Fabian Malekela na muuguzi, Joseph Raphael, ambao hivi karibuni
walikutana na Kingu aliyewataka warudi katika maeneo yao ya
kazi.
Pia alimuagiza Mratibu wa
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani humo, Manumbu Kalima, kuvunja mkataba na
Anna Malongo kwa kushindwa kutekeleza mkataba wa kuwahudumia
wananachi.
0 comments:
Post a Comment