LATEST POSTS

Thursday, March 13, 2014

Finyango mbili za nyama, zapelekea mtoto huyu kuchomwa moto mikono yake na baba yake mzazi. So sad eeh!

 
Mtoto Anjela Rashid[4]amechomwa moto mikono yote miwili na baba yake mzazi baada ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake huyo

Inasikitisha sana

Mtoto amelala bila ya uwangali zi wa mtu yeyote yule





Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema akihesabu mabati ili yauwze kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo

Hapa ndipo anapo lala mtoto huyo



Mabati yakitolewa ili yauzwe zipatikane fedha za matibabu ya mtoto huyo

Tukio la pili limetokea machi 8 mwaka huu mtaa wa Kanda ya juu kata ya Iduda ambapo mtoto Anjela Rashid[4]ameunguzwa na moto mikono yote miwili baada ya kula finyango mbili za nyama zilizopikwa na Baba yake.
Mama yake mzazi wa mtoto huyo hakuwepo wakati wa tukio hilo kutokana na kukimbia kwa mumewe Rashid Mwatiya[32] ambapo amekimbilia Sumbawanga Mkoani Rukwa majuma mawili yaliyopita ili kuwepa vipigo vya mara kwa mara alivyokuwa akipata.
Baada ya kutenda unyama huo Mwatiya alimfungia mtoto huyo ndani bila kumpatia matibabu yoyote na chakula kwa hofu ya kukamatwa kutokana na majeraha makubwa mikononi hali inayomfanya mtoto kushindwa kula chakula kwa kutumia mikono.
Kutokana na vidonda kutopatiwa matibabu vidole vimeanza kuoza na kutokana na maumivu makali mtoto amekuwa akilia mara kwa mara ndipo kilio hicho kilibainishwa na Balozi Shaban Tolinga ambaye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa lakini hakuchukua hatua zozote huku mikono ya mtoto ikioza.
Hata hivyo Mtendaji wa mtaa huo Emmanuel Malema baada ya kupata taarifa ya ukatili huo aliamua kufuatilia akiwa na waandishi wa habari ambapo mtoto alikuwa amelala sebuleni bila uangalizi wowote na njaa hali ilyomlazimu Mtendaji kuchukua mabati manne kuyauza ili kumpatia matibabu na chakula na kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
 
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Iduda amesema vitendo vya kikatili katika Kata yake vimekuwa vikifumbiwa macho kwa hofu ya kujenga uadui kwa watu wanaotoa ushahidi.
Aidha Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa amesema vitendo vya kiatili havita vumiliwa hivyo wananchi watoe ushirikiano ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekithiri kwa siku za hivi karibuni.
Chanzo: Mbeya yetu

0 comments: