John Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na
wakati wote kufungiwa ndani kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi
yake
|
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KWANI HATUNA JINSI IMEBIDI TUONYESHE KILA SEHEMU YA MWILI YA MTOTO HUYU KWA MATESO ALIYOKUWA AKIPATA HATA KUKAA ANASHINDWA |
Mwanahawa Nassoro[32] mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya Iyela. ndiye anaetuhumiwa kumtesa mtoto John Msumba |
Licha ya Asasi mbalimbali za kijamii kama TAMWA, GBV,TGNP
na Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto Mkoani Mbeya bado vitendo hivyo vimeendelea
kushamiri.
Katika matukio mawili yaliyotokea Jijini Mbeya hivi
karibuni yamewakumba watoto wawili wa wakazi wa Kata za Iyela na Iduda ambao
wamejeruhiwa vibaya kwa vipigo na kuchomwa moto na walezi
wao.
Tukio la kwanza limemhusisha mtoto wa kiume aliyefahamika
kwa jina la John Msumba[3]ambaye amekuwa akipigwa mara kwa mara na wakati wote
kufungiwa ndani kwa kufuli pia kunyimwa chakula na shangazi yake aitwaye
Mwanahawa Nassoro[32] mkazi wa mtaa wa Airport Kata ya
Iyela.
Vitendo hivyo vimetokana na kudaiwa mtoto huyo kujisaidia
hovyo hali iliyomletea usumbufu Mwanahawa ambapo mama yake hayupo na Baba mzazi
aliyefahamika kwa jina la Sumba Dinda akiwa machimboni wilaya ya Chunya
takribani miezi miwili iliyopita.
Sakata hilo lilibainika baada ya kutokea msiba mtaani
hapo Machi 12 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi mtoto huyo alipokuwa akilia
majirani walisogea eneo la tukio na kukuta mlango umefungwa kwa kufuli hivyo
kumlazimu Mjumbe wa mtaa Bi Rehema Mohammed kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa
huo Enock Mwampagama.
Mwampagama alitoa taarifa kwa Mtendaji wa mtaa Henry
Chaula ambapo walimkamata kwa mahojiano katika ofisi ya mtaa na baada ya maelezo
walimpeleka kituo cha Polisi Mwanjelwa kwa hatua
zaidi.
Uchunguzi umebaini kuwa mtoto huyo amekuwa akiteswa kwa
muda mrefu ingawa majirani na mwenye nyumba aliyefahamika kwa jina la Ollen
Kaguo hawakuweza kutoa taarifa ili kunusuru afya ya mtoto ambaye ameonekana kuwa
na ukosefu wa chakula bora na mwili ukiwa umejaa majeraha makubwa.
Chanzo: Mbeya Yetu
0 comments:
Post a Comment