LATEST POSTS

Thursday, March 20, 2014

MABAKI YA NDEGE YAONEKANA AUSTRALIA

Msemaji wa masuala ya usalama wa safari za ndege Australia, John Young, akiongea na waandishi wa habari.
Mabaki ya  ndege pichani ambayo kimoja kina ukubwa wa mita 24, yameonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.
Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya satelite ya…
Msemaji wa masuala ya usalama wa safari za ndege Australia, John Young, akiongea na waandishi wa habari.
Mabaki ya  ndege pichani ambayo kimoja kina ukubwa wa mita 24, yameonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.

Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana kama mabaki ambavyo huenda ni ya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13 zilizopita.
Waziri mkuu huyo, Tony Abbott, ameliambia bunge mjini Canberra kwamba picha za satelite zimeonyesha vitu viwili vinavyofanana na mabaki ya ndege hiyo.
Taarifa hii imejitokeza karibu wiki mbili baada ya ndege hiyo kutoweka na abiria zaidi ya 200 ikitokea mjini Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing.
Msemaji wa masuala ya usalama wa safari za ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vitu hivyo ambavyo kimoja kina ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.
Aliongeza kwamba, hata hivyo, huenda vitu hivyo si mabaki ya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa na ndege ya Australia katika neo hilo , ndege zaidi zinatarajiwa kuwasili katika eneo lenyewe na pia manowari ya jeshi inaelekea huko.

CHANZO: GPL

0 comments: