Bidhaa ya Mafuta ya mawese Mkoa wa Kigoma itapanda bei,kutokana
na Halmashauri ya wilaya hiyo, kukabidhiwa mradi wa Kiwanda kidogo cha kisasa cha uchakataji wa mafuta hayo.
Pia kujengwa kwa kiwanda hicho ni shabaha ya kupunguza changamoto ya uchakataji wa awali
ambao ulikuwa ukitumia nguvu na muda mrefu katika uchakataji wake, sambamba na
ubora usio na kiwango cha kuteka soko la
nje.
Akikabidhi mradi kwa Halmashauri,Meneja wa Mradi wa
uhifadhi Ziwa Tanganyika Seleboni Mushi alisema bidhaa hiyo itazidishwa
ubora na hivyo kuweka ushindani wa soko la nje na nchi za Bara la Asia,huku
akitaka halmashauri hiyo watumie sheria,kanuni na taratibu ili kiwanda hicho kiwe endelevu leo na siku zijazo.
Kwa Upande wa wachakataji wa zao hilo Fatuma Hamis na Rajabu Hassan
alisema kiwanda hicho ni tija kwao kutokana na ubora wa jengo na zana za kisasa
ambapo itasaidia kuongeza ujazo wa lita pamoja na ufungaji wa kisasa hali
itakayoongeza kipato kuanzia ngazi ya mkulima na mchuuzi wa mafuta hayo.
“hivi sasa bei ya soko la ndani tunauza dumu la lita 20 kwa
sh.21,000 lakini kupitia hii itapanda zaidi ya hapa kutokana na ubora wake na
kuongezeka kwa lita kutokana na kukamua makapi sahihi” alisema Hamisi
Naye Mgeni rasmi Katibu
tawala wa Mkoa Eng.John Ndunguru alisema ili kulinda mazingira maofisa kilimo
wa wilaya hiyo watumie mabaki ya mawese kwenye mfumo wa mbolea ambayo italeta tija
kwa wakulima wa kijiji hicho .
Mradi huo umefadhiliwa na GEF ,UNDP huku kiasi cha milioni 247.55 kimegharimu ujenzi
wa kiwanda hicho, wakilenga kupunguza changamoto ya uharibifu wa mazingira
katika mfumo wa ucheketaji wa kienyeji ambao hauna tija kwa wakulima na
wacheketaji wa mafuta hayo.
0 comments:
Post a Comment