Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe
Wakati serikali ya Uganda ikitangaza kwamba itafanya mazungumzo na mataifa ya Magharibi baada ya kutishia kusitisha misaada ya fedha kutokana na hatua ya Rais Yoweri Museveni kutia saini mswada wa sheria unaopiga marufuku ndoa za jinsia moja nchini humo, Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amemuunga mkono Rais wa Uganda kuhusu hatua yake hiyo ya kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Akizungumza katika ghafla ya sherehe ya harusi ya binti yake wa pekee, Rais Mugabe amesema haki ya binadamu ni mwanamke kuolewa na mwanaume, na sio kuolewa na mwanamke mwenzie, na hii ndio uvunjifu wa haki za binadamu.
Rais Mugabe amekua akiwashambulia sana wahusika wa vitendo vya ndoa ya jinsia moja, mara akiwaita, Mbwa, wakati mwingine Nguruwe. Mugabe amesema alikuwa hajui kama nchini mwake kuna shirika la mashoga, na aliambiwa hivi majuzi, uchunguzi unaenda kuanzishwa kujuwa ni kina nani.
Zimbabwe hairuhusu ndoa za watu wa jinsia moja kama ilivyo kwa jirani yake Afrika Kusini. Sheria ya kifungo chini humo inakataza ndoa za watu wa jinsi moja, na inaagiza kifungo cha mwaka mmoja na faini.
Serikali ya Uganda imejikuta matatani baada ya kupitisha sheria inayopiga marufuku ndoa za jinsia moja.
Tayari Marekani imetangaza kusitisha msaada wake wa Uganda kufuatia hatuwa hii, huku vitisho vikiendelea kutolewa na mataifa ya magharibi juu ya hatua hiyo.
Serikali ya Kampala sasa inasema itaanza kubana matumizi ya fedha katika Wizara mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment