Baada ya kusema hayo, niwashukuru sana Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Jaji Joseph Sinde Warioba kwa hotuba zao nzuri walizozitoa mbele ya
Bunge Maalum la Katiba, wakati wa uwasilishwaji wa rasimu na uzinduzi
rasmi wa chombo hicho.
Hakika, lilikuwa ni jambo la kufurahisha sana kuwaona viongozi hao
wakitoa hotuba ambazo ziliwavutia sana watu waliozisikiliza, kwani kila
mmoja alijenga hoja kwa umahiri wa hali ya juu, kiasi cha wananchi
kuzidi kuchanganyikiwa kuhusu mustakabali wa taifa letu, hasa kwa
masuala nyeti kama yale yanayohusu muungano wetu.
Kwa maoni yangu, wote wawili walikuwa na hoja kwa wanachokiamini,
kilichobaki ni kuwaachia wajumbe wa Bunge Maalum kuchuja pumba na
mchele, ili Mtanzania ale wali safi usio na chenga.
Hata hivyo, pamoja na wajumbe kuwa na jukumu hilo zito mbele yao,
bado hawa hawawezi kufanikiwa kama Mwenyekiti wao, Samuel John Sitta na
Makamu wake, Samia Suluhu Hassan hawatawaongoza kuijadili rasimu hiyo
kwa kufuata misingi ya haki, usawa na kuweka mbele masilahi ya nchi,
bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Sitta alijijengea heshima kubwa sana wakati akiwa Spika wa Bunge la
Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani aliliendesha vizuri, kwa
haki na bila upendeleo. Aliruhusu mijadala yenye tija kwa taifa na kamwe
hakuitetea serikali bungeni, licha ya ukweli kwamba chama chake ndicho
kiliunda serikali.
Lakini napenda kumweleza mzee Sitta kuwa Bunge la Katiba ni zaidi ya
lile alilomwachia mama Anne Makinda. Hili linazungumzia uhai wa taifa
letu, siyo tu kwa sisi tulio leo, bali kwa vizazi vyetu vijavyo. Ni
bunge la kihistoria na heshima aliyoipata ya kuliongoza, ni tunu ya
pekee kwake.
Ni lazima aelewe, ndani ya Bunge hilo kuna wajumbe kutoka makundi
mbalimbali, bila shaka kila moja litataka kuwasilisha na kutetea
masilahi yao binafsi, yenye kukidhi matakwa yao. Ni sawa, waache watetee
makundi yao. Sisi tunamtaka achuje, aweke mbele kwanza masilahi ya
taifa, kama alivyofanya wakati ule akiwa Spika.
Ni yeye pekee ndiye anayeweza kutuongoza kuelekea kupata katiba
tunayoitaka. Rai yangu kwake ni kumtaka kuwa makini kama wengi
wanavyomtarajia. Ninajua hata yeye ni mfuasi wa kundi mojawapo
linalotaka baadhi ya mambo yao yapitishwe. Ninaomba busara imuongoze
kutambua kuwa taifa lina maana zaidi kuliko chama chake cha siasa.
Aruhusu hoja zitawale, hata kama hazitalipendeza mojawapo ya kundi.
Asimamie kanuni vizuri na atoe nafasi hata ya wachache kusikika. Tunajua
bunge hili siyo la mwisho kuipitisha katiba mpya, kwa sababu baada ya
wao itabidi ipigiwe kura ya maoni na wananchi. Lakini endapo wao
wataikosea katika kuijadili na kuipitia, maana yake ni kwamba wananchi
watapigia kura katiba mbovu.
Ikipitishwa katiba mbovu, hii ndiyo itakayokuwa sifa ya Samuel Sitta,
kama mwenyekiti wa bunge hili. Vizazi vijavyo vitawahukumu wajumbe wa
bunge hili, hasa aliyewaongoza kupitisha kitu ambacho kitawaletea
matatizo badala ya manufaa kama tunavyotarajia.
Kwa hadhi aliyojijengea wakati ule akiwa spika, ni wazi kwamba
wananchi wana imani kubwa na utendaji wake na wengine wakaenda mbali
zaidi na kudai kuwa anafaa kuwa rais wa nchi. Hatutaki upendeleo, uoga
wala hujuma. Hatutaki mtu yeyote atoke ndani ya ukumbi huo baada ya kazi
yao kumalizika huku akijitangaza kuwa ameshinda.
Ikitokea kundi moja kujitangazia ushindi, tujue tumeshindwa kupata
katiba bora. Itapendeza siku ya mwisho, watu wote watoke wakitabasamu
kuonyesha wao kama taifa, wameibuka washindi! Lakini wakumbuke pia kuwa
wameahidi mbele ya Mungu kuwa watajadili bila upendeleo, atakaekiuka
atakuwa amemkufuru Mungu na asubiri mapigo yake.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la katiba, Mh. Samuel John Sitta.

0 comments:
Post a Comment