LATEST POSTS

Wednesday, March 12, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA
WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14



Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka
vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za
Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo
walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za
Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo
5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).
Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali
walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI (

www.pmoralg.go.tz) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi (

www.moe.go.tz) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.
Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye
Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi
mara moja.
Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za
kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili
kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka
ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.
Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila
sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi
hiyo.
Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri
umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu
kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu
atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa
kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu
anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo
vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa
uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya.
Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya
kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa
kurudi kwa waajiri wao na kuendelea na kazi.

IMETOLEWA NA
JUMANNE A. SAGINI
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAMISEMI

0 comments: