LATEST POSTS

Sunday, March 9, 2014

UPDATES: MAMA ALIYETOROKA NA MTOTO ALIYEUNGUA NA MOTO APATIKANA NJOMBE, NI BAADA YA TAARIFA HIZI KUSAMBAA

Huyu ndiye mama mkubwa wa mtoto Adolotea Nyavike, Bi. Salome Kiegu (35) ambaye alitoweka na mtoto huyo kusikojulikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.
 
Hatimaye mama aliyetoroka na mtoto aliyeungua moto apatikana baada ya kupiga simu Mbeya yetu Blog kuwa yupo Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo na kuomba radhi kuwa aliondoka bila kuaga na leo saa nane mchana atakuwa amerudi na mtoto huyo.
Mama huyo amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya Yetu kuandika mapema jana kwamba alikuwa
ametoweka bila taarifa zozote. Akiongea na Mbeya Yetu Blog amedai kwamba yeye aliondoka ili akashauriane na wazazi wa mtoto huyo ili waone ni jinsi gani watamsaidia lakini alipohojiwa amejikanyaga kanyaga na kuongea bila kuwa na uhakika na kile anachozungumza.
Hata hivyo baadaye atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli uko wapi kwa kuwa anatia
mashaka na maelezo yake. Tunaendelea kusisitiza kuwa kama kuna mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo ameonesha wasiwasi na kuondoa imani watu.
 
Chanzo: Mbeya Yetu Blog

0 comments: