LATEST POSTS

Sunday, March 9, 2014

Utata wa vitambulisho bandia wagubika tukio la kupotea kwa ndege ya abiria ya Malaysia


Ndege ya Malaysia iliyopotea
Ndege ya Malaysia iliyopotea

Juhudi za kutafuta ndege ya abiria ya nchini Malaysia ambayo haijulikani ilipo tangu ipoteze mawasiliano ikiwa na abiria 239 Ijumaa usiku hazijazaa matunda huku utata ukigubika vitambulisho vya abiria wawili ambao wanakisiwa kutumia vitambulisho bandia vilivyoibiwa Ulaya kupanda ndege hiyo.

 Kwa zaidi ya saa 30 baada ya chumba cha mawasiliano kupoteza mawasiliano na ndege hiyo boeing 777, wasiwasi umeongezeka kuhusu uwezekano wa kukosekana kwa usalama, huku mamlaka Kusini Mashariki mwa Asia zikisema kuwa bado hakuna dalili za kuonekana kwa ndege hiyo baada ya uchunguzi kuanza baharini.

Ndege hiyo MH370 ilipotea saa moja baada ya kuondoka mjini Kuala Lumper ikielekea Beijing nchini China ambapo raia 153 wa China walisafiri ndani ya ndege hiyo.
Idara za usalama nchini Malaysia zinafanya uchunguzi kuhusu uwezekano wa tukio la kigaidi kufuatia kupotea kwa ndege hiyo baada ya kubaini abiria hao wawili waliotumia vitambulisho bandia vilivyoibiwa Ulaya.
Chanzo: Rfi Swahili 

0 comments: