Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali
ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama
kwa kuyumba, akiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.
"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa
meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini
watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio
hilo la kutisha.
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini
kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli
kupinduka na kuzama.
Watu wawili wamefahamika kupoteza maisha na watu
mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa
sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi wa abiria wa meli hiyo ni
wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa
cha Jeju, nchini Korea Kusini.
Meli hiyo ilikuwa na watu 460.
0 comments:
Post a Comment