Home »
» Fun City, a nice place to visit in Dar-es-salaam
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN
CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya
Pasaka wakati wa mkutano alioufanya katika eneo la Fun City Kigamboni
jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake
imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita
tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea. |
|
Mitambo
ya kisasa iliyofungwa katika eneo la Fun City ambayo itawawezesha
wananchi kupata burudani kabambe zenye ubora wa kimataifa kwani hakuna
mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo. |
|
Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City, |
|
Moja ya Bwawa la kuongelea. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi akionyesha vigari vya mchezo. |
|
Bembea za kutosha. |
|
Bembea za watoto. |
|
Mapokezi ya Fun City. |
|
Eneo la Fun City linasehemu ya Ibada. |
|
Sehemu ya huduma ya kwanza nayo inapatikana hapa. |
|
Sehemu ya moja ya sehemu ya bembea za magari ikiongesha madhari nzuri za kiota cha burudani cha Fun City. |
|
Vigari vya umeme vinavyopita ndani ya maji. |
*YAFUNGA MITAMBO YA KISASA KWA AJILI YA MICHEZO YA KWENYE MAJI
Wakati Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni
ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo
yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa
kubwa la kuogelea.
Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharini.
Akizungumzia mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi
amesema, lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania
kufurahia michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.
Ameongeza kuwa mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo lake
itawawezesha wananchi kupata burudani kabambe yenye ubora wa kimataifa
kwani hakuna mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo inapatikana.
“Tumefunga mtambo huu ambao utakua ukitengeneza mawimbi ya aina sita
tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fan City, lengo
letu nikutoa burudani zaidi kwa watu wanaotembelea hapa”.Alisema Rizvi.
“Tumefanya uwekezaji wa mashine za kisasa za michezo mbalimbali kwenye
eneo letu ili kutoa burudani nzuri na za kipekee kwa wananchi
wanaotembelea eneo hili na hasa wakati huu wa Pasaka”. Alisisitiza
Rizvi. Fan City ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Fun City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia
na katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi,
Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo.
kutoka Urambonews.com
Kwa kweli hii ni sehemu nzuri sana kwenda kuitembelea. Siku moja nitakwenda na my hubby kuondoa stress.
0 comments:
Post a Comment