LATEST POSTS

Saturday, April 12, 2014

TASWIRA KUTOKA JNIA BAADA YA NDEGE YA KENYA AIRWAYS KUACHA NJIA JANA

Mmoja wa abiria katika ndege ya Shirika la Ndege la Kenya akitoka kwenye ndege hiyo.

HALI ya hofu ilitanda miongoni mwa abiria waliokuwa katika ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) hapo jana baada ya ndege hiyo kudaiwa kuteleza na kunasa njia kuu na kufanya ndege nyingine kushindwa kutua uwanjani hapo.

Chanzo cha ajali hiyo ni mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Abiria wapatao 49 pamoja na wafanyakazi 7 wametoka salama katika ndege hiyo wengine wakilazimika kutokea mlango wa dharura wakiwa wamelowa chapachapa. Uwanja ulifungwa kwa muda na baadhi ya ndege zililazimika kutumia Uwanja wa Zanzibar.

0 comments: