Watu 56 wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la 
Kenya(Kenya Airways) waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja 
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam(JNIA) jana
 ilipokuwa ikitua.
                
              
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Kamiishna 
Khamis Selemani alithibitisha kutokea kwa ajali akieleza kuwa 
ilisababishwa na rubani kupoteza mwelekeo na kushindwa kuona njia sahihi
 kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo.
                
              
Ndege hiyo yenye namba 5Y-FFT aina ya Embrarer 190
 yenye uwezo wa kubeba abiria 90 ilipata ajali hiyo mchana ikiwa na 
abiria 49 na wafanyakazi saba.
                
              
“Tulipata taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo 
majira ya saa 8:26 mchana. Ndege hiyo imepata hitilafu katika injini 
yake ya upande wa kulia ambayo imebonyea pamoja na kupasuka ubavuni,” 
alisema Selemani.
                
              
Kamanda huyo aliongeza kuwa pia tairi la mbele la 
ndege hiyo limepasuka baada ya kujigonga, lakini hakuna kifo 
kilichotokea wala majeruhi waliohitaji matibabu.
                
              
“Haitoweza kuruka kabla ya marekebisho kwani hewa 
itaingia ndani jambo ambalo haliruhusiwi kwa usafiri wa angani katika 
viwango vya kimataifa,” aliongeza Seleman.
                
              
Katika hatua nyingine, ndege ya Shirika la Ndege 
la Emirates, ilishindwa kutua kwenye uwanja huo jana kutokana na mvua 
hizo, hivyo kulazimika kwenda kutua Uwanja wa Ndege wa Mombasa nchini 
Kenya.






0 comments:
Post a Comment