LATEST POSTS

Tuesday, May 6, 2014

MAALIM SEIF,LIPUMBAA WAONGOZA MAZISHII YA SHEHE ILUNGA.....

     Waumini wa dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa Sheikh Hassan Ilunga kabla                    ya kumzika katika Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni jijini Dar es Salaam, jana.



KWA UFUPI
“Akiwa huko (India), alianza kutokewa na matatizo mapya ikiwa ni pamoja na baadhi ya viungo vyake kupooza au sijui tuseme kufa ganzi na mara ikawa leo mguu kesho unarudi hali ya kawaida na hali hiyo ikawa inajirudiarudia,” alisema.
Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad jana alikuwa miongoni mwa maelfu ya waumini wa Kiislamu waliojitokeza kumzika Sheikh Hassan Ilunga aliyefariki dunia Dar es Salaam juzi kwa maradhi ya kupooza.
Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF aliongozana na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba katika ibada ya kuaga mwili wa sheikh huyo, kabla ya maziko yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa.
Akizungumza kabla ya ibada ya maziko, Amiri wa Shura ya Maimamu, Sheikh Mussa Kundecha alisema marehemu alipata matibabu ya figo huko India na Aprili mwaka huu alirejea nyumbani.
“Akiwa huko (India), alianza kutokewa na matatizo mapya ikiwa ni pamoja na baadhi ya viungo vyake kupooza au sijui tuseme kufa ganzi na mara ikawa leo mguu kesho unarudi hali ya kawaida na hali hiyo ikawa inajirudiarudia,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Sheikh Kundecha alisema madaktari hawakubaini ugonjwa uliokuwa unamsumbua ndipo alipopewa ruhusa ya kurudi nchini.
“Aliporudi alikuwa anazungumza vizuri na kuwasiliana bila shida na watu wengine, ingawa kuanzia katika kiuno kwenda chini viungo havikuwa na mawasiliano mazuri na mwili,” alisema na kuongeza kuwa siku tatukabla ya mauti alipoteza fahamu.

0 comments: