" Safi sana in Joti voice". Sie kina yakhe tukafanye kazi wapi? Hii nimeipenda sana.
Serikali imesitisha ajira 70 za konstebo na koplo wa Uhamiaji
baada ya kuzuka kwa tuhuma za upendeleo uliokithiri wakati wa usaili.
Agizo hilo la Serikali lilitolewa jana na Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil ambaye ametengua kauli
yake ikiwa ni wiki mbili tu tangu alipozitangaza nafasi hizo.
Mara baada ya ajira hizo kutangazwa, wadau
mbalimbali walianza kulalamika kwa madai kwamba nafasi hizo zimetolewa
kwa upendeleo kwa ndugu na marafiki wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji.
Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani, Isack Nantanga ilisema Abdulwakil amesitisha
ajira hizo baada ya kuzagaa kwa tuhuma za upendeleo kwa ndugu na jamaa
wa watumishi wa idara hiyo.
“Kutokana na kusitishwa kwa zoezi hili, waombaji
wote walioitwa na kutakiwa kuripoti makao makuu ya Idara ya Uhamiaji
Agosti 5 mwaka huu sasa watatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa
tena.”
Ilisema Abdulwakil ameunda kamati ndogo kuchunguza tuhuma hizo na ikikamilika ndipo uamuzi utakapofanyika.
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tuhuma
zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
kwamba kulikuwapo na upendeleo wakati wa usaili.
Julai 13 mwaka huu, Idara ya Uhamiaji ilifanya
usaili wa kujaza nafasi 70 za mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waliopita ni 6,115 ambao walichujwa na kufika 1,681 walioingia katika kinyang’anyiro cha kusaka watumishi 70.
Utata ulivyo
Baadhi ya waliotakiwa kuripoti Agosti 5 mwaka huu
wanaodaiwa kuwa ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo ambao
majina yao yalisambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
ni: Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Amin Mandemla,
Alphonce Kishe – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Aleluya Kishe na Asha Burhani
Idd – ndugu wa Ofisa Uhamiaji na Tatu Burhani Idd.
Wengine ni Beatrice Temba – ndugu wa Ofisa
Uhamiaji, Joseph Kasike, Geofrey Justine Mhagama – ndugu wa Ofisa
Uhamiaji, Rose Mhagama, Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji,
Daniel Mgendi na Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Ofisa
Uhamiaji, Makwinya.
John Alfred Mungulu – mtoto wa Ofisa, Uhamiaji Alfred Mungulu,
Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji, Milambo, Michael J.
Choma – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, John Choma, Shimba H Zakayo – mtoto wa
Ofisa Uhamiaji, Zakayo Mchele na Upendo E. Mgonja - mtoto wa Ofisa
Uhamiaji Mgonja.
Wengine ni Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Ofisa
Uhamiaji, Adam Kidesu, Elizabeth Edward – ndugu wa Ofisa Uhamiaji,
Edward Martin, Ester Mahirane – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Mahirane na
Basil Lucian John – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Lucian.
Frank E Kajura- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Kajura,
Jacob P. Ulungi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Magnus Ulungi, Janeth John
Milinga – ndugu wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Milinga, Janeth R Lukuwi –
ndugu wa Ofisa Uhamiaji Eliza Lukuwi, Joseph N. Yondani – Mtoto wa Ofisa
Uhamiaji, Mary Yondani.
Leila Khatib Irovya - Mtoto wa Ofisa Uhamiaji
Abbas Irovya, Lucian F. Mlula – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Mlula,
Neema Kasian Lukosi- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Zubeda Abbas, Pendo D.
Gambadu – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Gambadu, Paschalia E. Mwenda – ndugu
wa Martin Edward Mwenda.
Theresia Ernest Kalunde – mtoto wa Ernest Kalunde,
Veronica G Vitalis – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Vitalis Mlay,
Victor G. Mlay- mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Vitalis Mlay na
Catherine J. Mapunda- mtoto wa Ofisa, Lucy Mapunda.
Uhamiaji wajitetea
Idara ya Uhamiaji imekiri kupokea malalamiko yaliyotolewa dhidi yake.
Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Rosemary Mkandala alisema jana kuwa wamepokea tuhuma hizo na wanazifanyia kazi.
“Ninaomba tu wale ambao walishiriki kwenye usaili
huo na wana malalamiko wayawasilishe rasmi ili tuweze kuyafanyia kazi.
Suala linachunguzwa sasa na matokeo yake yatabainisha kama kuna ukweli
au la,” alisema.
0 comments:
Post a Comment