Unajua watu wanaweza wakasema maneno mengi sana kuhusiana na mafanikio ya Diamond. Wapo watakaosema kuwa, mafanikio yake yanatokana na nguvu za giza ikiwemo U FREEMASON lakini kwa upande wangu mimi, kiukweli naona kabisa mafanikio ya Diamond yanachangakiwa pia kwa kiasi kikubwa na dua za mama yake mzazi ( Bi Sanura). Diamond amekua akionyesha heshima, kumheshimu na kumtunza mama yake kwa kadri Mwenyezi Mungu anavyomjalia. Matendo haya yanamfanya mama Diamond awe anamwombea mema mwanae kila siku hivyo Mwenyezi Mungu kuzidi kumfungulia milango zaidi ya mafanikio, kwani vitabu vya dini vinatuambia kwamba, tuwaheshimu baba na mama zetu ili tupate maisha marefu na heri duniani.
Hebu ona machozi ya furaha ambayo mama Diamond amelia baada ya kufanyiwa suprise ya gari na mwanae wakati wa birthday yake. Haya ni machozi ya heri na ama kwa hakika yanakwenda kufagia njia zaidi ya mafanikio kwa Mwanamuziki huyu.
Kwa mfano huu, ni vizuri sote tukajifunza namna nzuri ya kuwaheshimu, kuwatunza na kuwathamini wazazi wetu kwa kadri ambavyo Mwenyezi Mungu ametujaalia. Sio lazima tuwazawadie magari, la hasha kwani watu tunatofautiana vipato. hivyo, mthamini mama yako kwa kile ambacho Mungu amekubariki. Ama kwa hakika kwa kufanya hivi, tutapata kheri na miaka mingi duniani. Vinginevyo, tutamaliza waganga wote ulimwenguni na mafanikio tusiyaone kwani hakuna uchawi zaidi ya huu.
Kumbuka, mzazi anaweza kutoa machozi kutokana na matendo mabaya unayomfanyia, na anapolia kwa mabaya yako ujue ni laana kwako na pia mama anaweza kulia kwa mema unayomfanyia, na akilia kwa mema unayomfanyia hiyo ni baraka kubwa sana kwako. Hivyo, tuwaheshimu baba na mama zetu ili tupate heri duniani eeh!
Tukio la mama Diamond kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za
Amani, juzi Jumatatu, mishale ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza
jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.
SAPRAIZI YA NGUVU
Waalikwa na mama huyo, wote walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Waalikwa na mama huyo, wote walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Mmoja wa rafiki wa karibu na familia hiyo,
kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema kuwa hadi jioni,
mama Diamond hakuwa akifahamu kuwa aliandaliwa sherehe ya siku yake ya
kuzaliwa.
“Mipango
yote ilifanywa kwa siri mama Diamond hakujua kilichoendelea. Diamond
akiwa Marekani alitoa maelekezo mama yake afanyiwe shughuli hiyo hata
kama hayupo kwa sababu siku ya kuzaliwa haijirudii,” alisema rafiki
huyo.
KILICHOMLIZA
Muda
mfupi baada ya shughuli ya kufuturu kukamilika, mama Diamond alishangaa
kusikia kwamba kulikuwa na jambo jingine la ziada katika siku hiyo.
Alitolewa nje huku akiimbiwa ‘happy birthday’ ndipo alipogundua
kilichokuwa kikiendelea.
Mara baada ya shampeni isiyo na kilevi
kufunguliwa na waalikwa kupewa, meneja wa Diamond, Babu Tale na wapambe
wengine walimuongoza mama huyo hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus
Harrier na kuelezwa kuwa ni mali yake kuanzia muda huo tamko
lililomshtua na kuanza kulia akiwa haamini alichosikia!
“Siamini macho yangu, siamini... asante sana mwanangu (Diamond),
nakuombea kila kukicha mwanangu uwe na afya njema, unilee kwa upendo,
asante Mungu,” alisikika mama Diamond akitamka kwa sauti iliyoambatana
na kilio cha nguvu.
Muda huohuo akafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari hilo lililopambwa ndani kwa vitu kibao vya thamani.
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA Machozi ya mama Diamond
hayakukoma hata baada ya kushuka ndani ya gari, alionekana
kuchanganyikiwa kama siyo kutoamini sapraizi ya mwanaye, ndipo Miss
Tanzania 2006, aliye pia mchumba wa mwanaye, Wema Sepetu na staa wa
filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.
Mastaa hao ambao ni mtu na shogaye,
walimchukua mwanamke huyo na kwenda naye pembeni ambako walimsihi atulie
na akubaliane na alichokiona kwani ndiyo ukweli wenyewe.
Juhudi zao zilizaa matunda, kwani muda
mfupi baadaye mama Diamond alifuta machozi na kurudi katika hali yake ya
kawaida ingawa alishindwa kuficha furaha yake.
THAMANI YA GARI
Akizungumzia thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni 34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo kununuliwa.
Akizungumzia thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni 34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo kununuliwa.
“Hiyo milioni 34 ni pamoja na muziki unaouona ndani ya gari, hizi
skrini tatu na mazagazaga mengine kama mnavyoona,” alisema Babu Tale
huku akiwaonesha waandishi wetu.
DIAMOND BONGO
Hadi tunakwenda mitamboni, Jumanne usiku, ilielezwa kuwa, Diamond alitarajiwa kutua jana Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Marekani alipokuwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za BET.
Hadi tunakwenda mitamboni, Jumanne usiku, ilielezwa kuwa, Diamond alitarajiwa kutua jana Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Marekani alipokuwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za BET.
Habari kutoka ndani ya familia zilieleza kuwa, nyota huyo naye
ameandaliwa sapraizi ya nguvu kutoka kwa kampani yake wakishirikiana na
familia. “Wamejiandaa vya kutosha kumfanyia saprazi ya nguvu na yeye
mara tu atakapotua Bongo. Wanafanya siri sana, haijajulikana atafanyiwa
nini,” kilipasha chanzo chetu.
Nyota ya Diamond imeonekana
ikiwaka sana siku za hivi karibuni ambapo amekuwa akipiga shoo za mara
kwa mara katika nchi mbalimbali huku akishirikishwa kwenye tuzo za ndani
na za kimataifa.
0 comments:
Post a Comment