NAIBU Waziri wa Maji, Mheshimiwa Amos Makalla amegeuka mbogo kufuatia madai ya kukwepa kodi kupitia gari analodaiwa kulimiliki aina ya Toyota Dyna lililokamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani Mvomero mkoani Morogoro hivi karibuni.
Akizungumzia habari zilizoandikwa na gazeti moja linalotoka kila siku
nchini kukanusha tuhuma hizo, Makalla alisema licha ya kuwa yeye siyo
mmiliki wa gari hilo lenye namba za usajili T534 BFP, lakini pia siku
lilipokamatwa, tayari lilishalipiwa leseni ya barabara.
“Hizi ni mbinu chafu za kunichafua, siwezi kutoa misaada ya mamilioni
kwa wapiga kura wangu halafu nikashindwa kulipa shilingi laki sita.
Mimi siyo mmiliki wa hilo gari, ninaitwa Amos Gabriel Makalla, kadi ya
gari imeandikwa Gabriel Amosi Makalla, wanajua siyo langu lakini
wananichafua makusudi.
“Halafu kitu kingine ni kwamba gari lile limekaa gereji kwa muda
mrefu sana na kwa sababu hiyo lisingeweza kulipa leseni ya barabara
wakati halitembei, limekaa kule zaidi ya mwaka mzima. Hizi ni siasa za
kuchafuana na hakika siwezi kukubali.
“Nimemuagiza mwanasheria wangu ashughulikie suala hili, habari hiyo
siyo ya kweli, hainihusu na imelenga kunishushia heshima na kwa maana
hiyo ninawadai kunilipa shilingi bilioni moja kwa sababu hadi wanaandika
habari hiyo, gari hilo halikuwa linadaiwa,” alisema Makala.
0 comments:
Post a Comment