Waheshimiwa Madiwani Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM) wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe.Alhaji Adam H.Malunkwi, kwa kushirikiana na Wataalamu wa Halmashauri walifanya ziara ya kutembelea vyanzo vikubwa vya Halmashauri yao hasa kwa upande wa Minada. Lengo kuu la ziara yao lilikuwa ni kufanya tathmini ya kujua kiasi cha Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo ambao huuzwa/kununuliwa kwa kila mnada mmoja katika minada hiyo sambamba na kujionea changamoto ambazo zipo katika minada hiyo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi ili kuboresha vyanzo hivyo ili hatimaye kuweza kuongeza kiasi cha mapato kutoka katika vyanzo hivyo. Ziara ilianza tarehe 25-28/3/2013. Chini ni picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara hiyo.
MNADA WA KIN'GWANGOKO ULIOPO KATIKA KATA YA SASU,TARAFA YA KALIUA.
Wananchi wakijipatia mahitaji mbalimbali katika soko la King'wangoko alamaarufu kama kona nne. Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Ulyankulu na pia wapo ambao hufika hapo wakitokea Kahama, Mwanza n.k
Wale wa mnada nao hao
Biashara ya N'gombe inaendelea
Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalamu wa Halmashauri wakipata maelezo kuhusiana na hali ya mnada wa King'wangoko na changamoto zake kutoka kwa Wakala wa Ushuru wa Mnada huo na Afisa Mifugo wa eneo hilo.
Theresia Chacha
Mwandishi.
0 comments:
Post a Comment