LATEST POSTS

Sunday, March 10, 2013

MHESHIMIWA KADUTU ATOA MSAADA WA JEZI ZA MPIRA NA MIPIRA KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA LAPTOP KWA MWANDISHI WA VIKAO


Diwani wa Kata ya Ichemba Mhe.John Kadutu atoa msaada wa Jezi za Mpira kwa Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe. Alhaji Adam Malunkwi Diwani wa Kata ya Uyumbu na Msaada wa Laptop kwa Mwandishi wa Vikao vya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw. Boniventure Soffu.
 
                
Mheshimiwa Kadutu Diwani wa Kata ya Ichemba mwenye miwani akimkabidhi Mwandishi wa Vikao Bw. Soffu Alloyce msaada wa Laptop. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Alhaji Adam Malunkwi akishuhudia.
 

                                                Bw. Soffu akiifurahia zawadi yake


                 Mheshimiwa Kadutu akimpa maelekezo Bw. Soffu ya namna ya kuitumia laptop hiyo
 
 
                                           Darasa la matumizi ya laptop hiyo linaendelea
 

Alhaji Adam Malunkwi (wa Katikati) akipokea msaada wa jezi kutoka kwa Mheshimiwa Kadutu. wa Kwanza kushoto ni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Haruna Kasele.

                                                   
                                                 Kamata na hizi Mheshimiwa Mwenyekiti

 
                                                                        Na hizi tena
 

 
                                                                          Na soksi
 
Mheshimiwa Kadutu akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
 
Kama mwandishi, napenda kumpa pongezi nyingi Mheshimiwa Kadutu kwa moyo wake wa kujitolea na kikubwa zaidi huwa habagui. Yeye hutoa msaada kwa yeyote bila kujali ni mwananchi anayetoka katika Kata yake au la. Big UP sana Mheshimiwa Kadutu. Mungu akuongezee zaidi. Ubarikiwe sana.
 
Theresia Chacha.
 
 
 

0 comments: