OKTOBA 25, mwaka huu ilikuwa ni moja kati ya siku za kihistoria nchini kwa Watanzania wote kujumuika na kupiga kura za kuwachagua wabunge, madiwani na rais.
Siku
hiyohiyo pia katika Jiji la Milan, Italia kulikuwa na tukio la
kihistoria kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla katika Tuzo
za MTV Europe Music (EMA) na kufanikiwa kuibuka na ushindi kupitia
kipengele cha Best Worldwide Act: Africa/India ambacho alikuwa akichuana
na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia
Miss World mwaka 2000.
Uso kwa uso na mastaa ulaya
Kati ya matukio ambayo Diamond anasema hawezi kuyasahau ni pamoja na
kupata shavu la kukutana na mastaa kibao wa ulaya ambao walipafomu na
wengine kuchukuwa tuzo.
“Nimekutana na mastaa wengi ambao sikuwahi kukutana nao kabisa zaidi
ya kuwaona tu kwenye mitandao na TV. Mastaa hao ni pamoja na Jason
Deluro ambaye pia alipafomu Wimbo wa Want to Want, Pharrel Williams naye
alipafomu Wimbo wa Freedom.“Nilipata bahati pia ya kuwashuhudia mastaa
wengine kama vile Justin Bieber, Ed Sheeran na wengine kibao,” alisema
Diamond.
Bieber anyakua 5 kwa mpigo
Staa wa Pop, Justin Bieber aliweka historia kwake katika tuzo hizo baada ya kuibuka na tuzo tano kwa mpigo.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao.
Wazungu wapagawa na Diamond
Katika hali ya kushangaza mapema kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za
utoaji tuzo, Diamond aliyekuwa amevalia suti nyeupe alitinga ‘red
carpet’ na kushangaa kuvamiwa na wazungu waliookuwa wamepanga foleni
kuwasubiri mastaa huku kila mmoja akiwa na simu yake mkononi akitaka
kupiga picha naye (selfie).
Washindi waliopita
Katika kipengele alichoshinda Diamond, alitanguliwa na Abdelfattah
Grini (Morocco) aliyechukuwa mwaka 2011, Ahmed Soultan (Morocco) mwaka
2012 na 2013 na wa mwisho alikuwa Mohamed Assaf (Palestina).
Diamond anasemaje?
Kutokana na ushindi huo uliokuja Tanzania na Afrika kwa ujumla,
Diamond alifunguka mengi ya kushukuru kwa wale wote waliompigia kura na
kuahidi kufanya makubwa zaidi ya hayo katika kazi zake za muziki.
“Nimeshangazwa sana kwa namna ambayo nimepokelewa kwa kishindo nchini
Italia. Wazungu wamenionesha thamani ya juu kwa mapokezi makubwa na
kunishangilia na kunipongeza kwa tuzo niliyoipata. Nasema asanteni sana
Watanzania wenzangu kwa sapoti mlionionesha mwanzo mwisho hadi kwa
kunipigia kura na kufanikiwa kuibuka mshindi kutoka Afrika,” alisema
Diamond.
Diamond alifanikiwa kupita tano bora Afrika katika Tuzo za Ema baada
ya kupigiwa kura za kutosha na mashabiki wake kupitia mtandao wa
Twitter. Wasanii wa Afrika aliokuwa akichuana nao kabla ya kutua Italia
ni Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na
Wizkid (Nigeria).
Kutoka www.urambonews.com
Nakupongeza kwa ushindi wa tuzo hii Diamond. Hakika unaendelea kupeperusha vyema nchi yetu ya Tanzania. Mwenyezi Mungu azidi kuwafungulia milango na wasanii wengine wote ili nchi yetu izidi kung"ara zaidi.
0 comments:
Post a Comment