Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema, Chiku Abwao )kushoto)
akuongea na wafuasi wa ACT - Wazalendo baada ya kupitishwa na chama
hicho kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini
Kada aliyewania ubunge kupitia Chadema katika Jimbo la Kalenga na kutemwa kwenye kura za maoni, Mwanahamisi Muyinga ameibuka mshindi wa kura hizo katika jimbo hilohilo kupitia chama cha ACT-Wazalendo.
Katika
uchaguzi uliofanyika katika Kata ya Mlandege mwishoni mwa wiki
iliyopita, Muyinga aliibuka mshindi kwa kupata kura 10 akifuatiwa na
Daniel Mwangili aliyepata kura saba, huku Edward Mtakimwa na Kiduo
Mgunga wakipata kura tatu kila mmoja.
Mbali na Muyinga,
wengine waliotemwa Chadema na kushinda ACT ni aliyekuwa Diwani wa Kata
ya Kunduchi, Janeth Rithe na Dickson Ngh’illy aliyewahi kugombea Jimbo
la Temeke mwaka 2010. Ofisa wa Habari wa ACT- Wazalendo, Abdallah Khamis
alisema jana kuwa Ngh’illy ameshinda katika jimbo jipya la Kibamba
baada ya kupata kura 19 kati ya 29 zilizopigwa. Alisema kabla ya kura
hizo kupigwa, mgombea mmoja alijitoa na kuacha nafasi hiyo ikiwaniwa na
Ngh’illy, Monalisa Ndala na Edna Mwango aliyeambulia kura mbili. “Rithe
ameshinda baada ya kupata kura 38 kati ya 58 Jimbo la Kawe, huku Mohamed
Ngulangwa akiibuka kidedea Jimbo la Temeke baada ya kupata kura 80 kati
ya 93,” alisema Khamis.
Akizungumza mara baada ya
kutangazwa mshindi, Muyinga aliwashukukuru wapigakura na wakazi wa
Kalenga kwa kumuamini na kumpa fursa ya kupeperusha bendera ya chama
hicho na kwamba hatawaangusha.
“Nawashukuru kwa kunipa
heshima hii. Nataka kuwaeleza kuwa mimi natoka ukoo wa machifu, nimeomba
ruhusa ya kuifanya kazi hii katika Jimbo la Kalenga na nimeruhusiwa,”
alisema Muyinga na kuongeza:
“Nawafahamu wakazi wa
Kalenga kwa zaidi ya asilimia ya 90. Najua kuwa wanategemea kilimo na
mimi nimesoma mambo ya kilimo, nitatumia taaluma yangu kuwaletea
maendeleo.”
0 comments:
Post a Comment