LATEST POSTS

Thursday, January 3, 2013

MAANDALIZI YA UGENI WA MHE:RAIS JAKAYA KIKWETE WILAYA YA URAMBO NA KALIUA

Kiongozi nambari 1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuja katika Wilaya zetu za Urambo na Kaliua mapema wiki ijayo. Katika ziara yake, Mheshimiwa Rais atazindua shule ya Sekondari ya Kaliua ( Maabara tatu) na kutembelea eneo ambalo litakuwa ni ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Aidha, Rais atapata wasaa/ fursa ya kuongea na Wananchi wa Wilaya hizi katika maeneo ambayo yamepangwa.
Kama ilivyo ada, huyu ni mtu mkubwa sana hivyo Viongozi wa Halmashauri kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini kila mmoja kwa upande wanafanya maandalizi ili kuhakikisha kuwa, kiongozi wetu huyu anakua comfortable katika kipindi chote atakachokuwepo hapa Urambo na Kaliua.

Karibu sana Wilayani kwetu ( Urambo na Kaliua) Mheshimiwa Rais. Tunaimani kubwa na wewe na Wananchi wako wanamatumaini makubwa sana na wewe. Wanakusubiri sana Rais wao kipenzi. Rais wa watu.

Matukio yanayojiri Wilayani kila mmoja kwa sekta yake.

                               MAFUNDI WA AC WAKIFANYA VITU VYAO





                          WA USAFI WA MAZINGIRA NAO HAWAKO NYUMA












                                     
                                    WA KUPAKA RANGI NAO WAMO

 

0 comments: