LATEST POSTS

Tuesday, July 16, 2013

JOAN, HADIJA MNOGA KIMOBITEL NA PAULINE ZONGO WAUNDA KUNDI JIPYA LA MUZIKI LINALOITWA NDEGE WATATU


Wanadada watatu ambao wapo katika fani ya muziki kitambo wameamua kuungana na kuunda kundi la muziki liitwalo ndege watatu. Wanadada hao si wingine bali ni Hadija Mnoga (Bundi), Joan Matovolwa (Tausi) na Pauline Zongo ( Kasuku) . Wakiongea kwa kujiamini katika kipindi cha Hot Mix cha Channel 5 cha tarehe 15 Julai,2013, wanadada hao wamesema kuwa, wapo kamili na wamejipanga hasa katika game kwani wamewasoma mashabiki wanataka nini kwa sasa.
Aidha, wanadada hao wamewahakikishia mashabiki wao kwamba, kundi lao hilo halitaweza kuvunjika kwani wao ni marafiki wakubwa tena wa muda mrefu hivyo wanajuana vema lakini pia wanamtanguliza Mungu katika kazi zao za kila siku kwani bila Mungu, Mwanadamu pekee hawezi.
Urambonews inawatakia kila rakheri Ndege watatu na inshallah, Mwenyezi Mungu atawajalia katika safari yao waliyoianza. Na kilichonifurahisha ni kuona kwamba wanajiamini na wamedhamiria kufanya hilo walilokusudia kulifanya. Kikubwa ni kuvumiliana na kuepuka maneno maneno ya watu ambayo yanaweza yakawatenganisha.
Tayari kundi hilo limeachia wimbo wao unaoitwa Misukosuko ya mapenzi ambao umeanza kupigwa katika vituo kadhaa. Hongereni wadada kwa maana mmejaaliwa sauti tamu kwelikweli. Kazeni buti
 

Joan
 

Hadija Mnoga
 
 
Pichani kutoka kushoto ni Joan, Hadija Mnoga na Pauline Zongo wanadada wanaounda kundi la Ndege watatu
 
 
 

0 comments: