Hivi karibuni, Wajumbe wa Kamati ya mfuko wa Jimbo la Uramb Magharibi wakiongozwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi Bw. Masebo walifanya ziara ya kuhakiki wanafunzi ambao wanasomeshwa na mfuko huo ili kuona mahudhurio pamoja na maendeleo yao shuleni. Mbunge wa Urambo Magharibi Mhe. Juma Kapuya, kupitia mfuko wa jimbo la Urambo Magharibi, pamoja na kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa jimboni mwake, vilevile mfuko huo unasomesha jumla ya wanafunzi 228 wanaosoma katika shule kumi na nne zilizopo katika jimbo lake ambapo jumla ya shilingi 6,222,502.00. Shule hizo ni Sekondari ya Ushokola,
Kazaroho, Kaliua, Kapuya, Ugunga, Igagala, Uyowa, Ukumbisiganga, Mwongozo,
Mkindo, Uyumbu, Usinge na Kashishi.
Wajumbe wa Kamati ya mfuko wa Jimbo Urambo Magharibi wakiongea na Mkuu wa shule ya Kaliua Sekondari kuhusu wanafunzi wanaosomeshwa na Mfuko huo.( Kaliua Sekondari ni moja kati ya shule za Mkoa wa Tabora ambayo inafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa na pia, Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete alizindua maabara tatu ya Kemia, Fizikia na Baiolijia mapema januari mwaka huu)
Wanafunzi wa Kaliua Sekondari wanaosomeshwa na Mfuko wa Jimbo la Urambo Magharibi wakiwa katika picha Wajumbe wa Kamati ya Mfuko huo walipofika shuleni hapo kukagua mahudhurio na maendeleo yao shuleni.
Mandhari ya Kaliua Sekondari
Mandhari ya shule inavutia
Hapa Wajumbe wakiongea na Mkuu wa Shule ya Kapuya Sekondari
Wanafunzi wanaosomeshwa na Mfuko wa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi katika shule ya Kapuya Sekondari
Wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Urambo Magharibi
Mjumbe (Eng. Justin Lukaga) akikagua vitabu vilivyonunuliwa kwa fedha za mfuko huo katika Shule ya Sekondari ya Kapuya.
Bw. Masebo(menye shati la draft) ambaye ni Katibu wa Mbunge akiangalia vitabu ili kujiridhisha. Mwanamama aliyeinama ni Mkuu wa shule ya Kapuya Sekondari.
Sehemu ya vitanda vilivyonunuliwa kwa fedha ya Mfuko wa Jimbo la Urambo Magharibi katika sekondari ya Mwongozo Ulyankulu.
Picha ya Katibu wa Mbunge, Mjumbe wa Kamati na Wanafunzi wanaosomeshwa na Mfuko wa Jimbo Mwongozo Sekondari
Wanafunzi wa kazaroho Sekondari
Katibu wa Mbunge jimbo la Urambo Magharibi Bw.Masebo akiwasisitiza wanafunzi kusoma walipofika Igagala Sekondari.
Wanafunzi wa Ushokola Sekondari pamoja na Mwalimu Mkuu wao wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe
Hapa mfuko ulichangia ukarabati wa sakafu ya darasa
Msaada wa Kisima cha Maji katika Sekondari ya Ushokola
Mwalimu akifurahia maji
Wote ni full vicheko, ni kama wanasema asante mfuko wa jimbo kwa kutuchimbia kisima.
0 comments:
Post a Comment