Baada ya mchakato wa muda mrefu, hatimaye Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imegawanywa rasmi Urambo kuwa Wilaya mbili ya Urambo na Kaliua mnamo tarehe 5 Agosti 2013 lengo likuwa ni kuhakikisha kuwa, Serikali inasogeza huduma kwa Wananchi.
Baada ya mgawanyo huo kufanyika, kila Wilaya sasa inatakiwa kuchagua uongozi wake wa Halmashauri kwa maana Wilaya ya Kaliua inatakiwa ichague Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na Makamu wa Halmashauri pamoja na Wenyeviti wa Kamati za kudumu wakati Wilaya ya Urambo inatakiwa ichague Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Wenyeviti wa Kamati za kudumu kwa kuwa tayari inaye Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kwa upande wa Wilaya ya Urambo, tayari imeshafanya uchaguzi siku ya tarehe 11 Agosti, 2013 katika Ukumbi wa FDC Urambo na kupata Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Elia P.Kafwenda ambaye alipata kura 13 kati ya kura 21 na Mpinzani wake Mhe. Amatus Ilumba alipata kura 8 kati ya kura 21.
Urambonews.com inampongeza Mhe. Elia Kafwenda kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na inamwombea kwa Mungu ampe hekima na uadilifu katika kuingoza Halmashauri ya Urambo. Pia, Wenyeviti wote wa Kamati za kudumu Mungu awatangulie.
Tunasubiri uchaguzi wa Kaliua. Tutawajulisheni yatakayojiri.
Mhe:Elia Kafwenda (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo (katikati) Mhe. Anna Magowa mara baada ya uchaguzi.
Waandishi wa Habari nasi hatukuwa nyuma. Tulikuwa tupo tukifuatilia mchakatop mzima wa uchaguzi unavyokwenda
Mchakato wa upigaji kura ukiendelea
Wataalam wakifuatilia mchakato wa uchaguzi
Kura zikihesabiwa
Makamu Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mhe.Elia Kafwenda akiwashukuru wajumbe mara baada ya uchaguzi
Wajumbe na Wataalamu wa Halmashauri wakiwa nje ya ukumbi wa FDC Urambo mara baada ya uchaguzi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment