LATEST POSTS

Sunday, August 18, 2013

TANZANIA SIO SHABA LA BIBI ASEMA RAISI KIKWETE

 
Akihutubia kuhusiana na suala la Wakibizi, katika kipindi maalum TBC siku ya Ijumaa saa nne kamili usiku, Raisi Jakaya Kikwete alisema kuwa, isifikie mahali Watanzania washindwe kutembea bila ya kusindikizwa na polisi kwenye Nchi yao.
Raisi Kikwete aliendelea kusema kuwa, chanzo cha kuharibika kwa hali ya usalama Nchini Tanzania ni Wakimbizi.
Kuhusu suala la Wahamiaji haramu Rais alisema mtu hawezi kuhoji dhamira ya Tanzania kuhusu Wakimbizi.
Alisema, jumla ya Wakimbizi laki moja na elfu sitini wamepewa uraia hivyo waliopo tofauti na hao si halali. 'Tuliwapa fursa lakini walishindwa kuitumia". Alisema Raisi Kikwete.
Alisisitiza taratibu za Nchi zifuatwe na sio watu waingie na kutoka nchini kiholela.kwani Tanzania sio shamba la bibi. Raisi amewataka Maafisa uhamiaji wawe makini na wachukue hatua kwa wote wanaoruhusu wakimbizi kuingia nchini kiholela kwani Watendaji wamekuwa wakiingilia majukumu ambayo siyo yao.
'Hatuzii mtu kuingia nchini ila kinachotakiwa ni kufuata na kuheshimu taratibu za nchi".

0 comments: