LATEST POSTS

Wednesday, November 20, 2013

UGONJWA WA HEPATITIS B UPO NA UNAUA, NENDA KAPIME SASA

Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano
 
Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano.
HEPATITIS B NI NINI?
Hepatitis B ni ugonjwa wa manjano ambao hushambulia ini.
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye KIFO.
Inakadiriwa watu milioni 350 duniani wameathirika na ugonjwa huu ambapo watu 620,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huu.
HEPATITIS B UNASABABISHWA NA NINI?
Ugonjwa huu husababishwa na virusi waitwao Hepatitis B (HBV) ambao hukaa katika ini, damu na baadhi ya majimaji mwilini.
             Virusi vya Hepatitis baada ya kulishambulia ini.
UNAAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia zifuatazo:
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki
Mojawapo ya njia zinazoambukiza ugonjwa wa Hepatitis B.
NB: Ugonjwa huu hauambukizwi kupitia chakula, maji au kushikana mikono na waathirika.
DALILI ZAKE
Dalili za ugonjwa huu huchukua muda mrefu kuonekana, zikionekana mgonjwa anakuwa tayari ameathirika sana na ni kama ifuatavyo:
-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi
           Daktari akifavya vipimo vya ugonjwa wa Hepatitis B.
KINGA
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama
          Mgonjwa wa Hepatitis B akipandikizwa ini na madaktari.
TIBA
-UGONJWA HUU HAUNA TIBA, japo mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kushambulia ini.
-Kupandikiza ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa ini lingine japo ni vigumu kupata ini salama.
-Mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia pombe, madawa ya kulevya na vitu vingine vinavyochosha ini.
SOURCES: GLOBAL PUBLISHERS

0 comments: