Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.…
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwasili katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara leo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa maadhimisho ya sherehe za uhuru wa miaka 52 ya Tanzania Bara.
Vikosi mbalimbali vya majeshi vikipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete kutoa heshima zao.
Rais Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Picha ya Rais Shein iliyotengenezwa na vijana.
Wananchi wa Tanzania Bara (Tanganyika) leo wameadhimisha miaka 52 ya uhuru wake uliopatikana Desemba 9, 1961. Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam amabapo mgeni rasmi alikuwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Viongozi mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.
Chanzo: Global publishers
0 comments:
Post a Comment