Kilima cha Kanyama lilicho sababisha mauti, kilichokuwa kinamilikiwa na marehemu Mabina kwa kuridhiwa na serikali ya kijiji iliyotoa hati ya umiliki. |
Njia yenyewe ndiyo hii ambayo pia marehemu aliitumia kupita wakati akikimbia kujiokoa baada ya kundi la watu waliokuwa wakishambulia. |
Ni kona ambayo ndipo shambulizi lilianzia huku marehemu akijivuta taratibu kuelekea eneo la msaada. |
Marehemu alifika eneo hili akijaribu kukimbilia katika moja ya nyumba zinazo onekana mbele ili kupata msaada wa kujiokoa. |
Lakini kabla hajafika katika nyumba hizo eneo lililo zungushiwa duara ndipo alipo anguka baada ya kupigwa jiwe kichwani na kuanguka chini nakuanza kushambuliwa kwa mawe hadi mauti yalipomkuta. |
Kwa ukaribu zaidi na pembeni ni baadhi ya mawe yaliyo tumika kumshambulia. |
Ndivyo alivyokutwa na mauti mwenyekiti huyo wa zamani CCM. |
Nyumbani kwa marehemu na sehemu ya waombolezaji. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kulia) pamoja na Mkuu wa Usalama mkoa (kushoto) wakimfariji mjane wa marehemu Clement Mabina. |
Baadhi ya waombolezaji. |
Huzuni kubwa imetawala kwa wafanyakati wa Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) nyumbani kwa marehemu. |
Watu
hao wamekamatwa wakati hofu ikiwa imewakumba wakazi wa maeneo ya Kisesa
na Kanyama, eneo ambalo marehemu Mabina aliuawa na watu wenye hasira
katika kile kilichoelezwa kuwa mgogoro wa mashamba.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
SACP,Valentino Mulowola, akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya
simu, alisema hadi sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo.
Alisema
watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti jana,ambapo jeshi hilo
linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika katika
mauaji ya Mwenyekiti huyo wa zamani wa CM Mkoa wa Mwanza.
“Tunaendelea
na upelelezi wa tukio hili la mauaji ya kinyama ili hatua za kisheria
zichukuliwe kwa wahusika na kuna maendeleo mazuri.Tuna washikilia watu
saba wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo,” SACP Mulowola
Katika
tukio hilo la mauaji, Mabina aliuawa kwa kukatwa mapanga na kupigwa
mawe ambapo alikutwa na majereha makubwa kichwani kichogoni.
Kabla
ya kuawa na wananchi hao,marehemu alimpiga risasi mtoto Temeli Malemi
kwa (11) bahati mbaya wakati akijihami na mashambulizi ya wananchi hao.
Ilielezwa jana na Kamanda wa Polisi SACP Mulowola kuwa marehemu alikutwa na silaha mbili aina ya Short-gun na bastola moja.
Hata
hivyo ndugu wa marehemu walishindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa
habari kuhusiana na habari zilizoandikwa na mitandao ya kijamii
ikihusisha kifo cha Ndugu yao (Mabina) na masuala ya kisiasa.
Aidha
habari kutoka eneo la tukio mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa alikutwa
na simu ya mkononi ya marehemu,hata hivyo kamanda hakutaka kutaja jina
lake na watuhumiwa wengine kwa madai ya kuwa kutaja majina kungeweza
kuvuruga upelelezi.
taarifa
za baadhi ya watu waliokuwa wakinong’ono kuwa kundi linalosadikiwa
kuhusika na mauaji hayo lilijiandaa kufanya kitendo hicho cha kinyama.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kuwa tayari hofu kubwa na taharuki imewakumba
wakazi wa kijiji cha Kanyama na baadhi wameyakimbia makazi yao wakihofia
kukamatwa.
Kwa
upande wa familia , mdogo wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Timoth
Grigory Mabina alisema kwamba tangu kutokea kifo cha Kaka yake kumekuwa
na upotoshwaji wa taarifa za tukio hilo unaofanywa na mitandao ya
kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuripoti kwa utashi wa
kisiasa zaidi kuliko ukweli.
Akizungumza
nyumbani kwa marehemu alisema kuwa taratibu za mazishi bado zinaendelea
ikiwa ni pamoja na kuwasubili watoto wawili wa marehemu walioko nje ya
nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evarist Ndikilo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo akiwa nje ya Mkoa huo
alipokea kwa maskitiko makubwa na kushangazwa na watu ambao walitekeleza
unyama huo baada ya kuamua kujichukulia sheria mkononi.
Mhandisi Ndikilo alisema kwamba
serikali inaendelea kufanya uchunguzi wake kupitia vyuombo vya dola na
kutoa wito kwa wananchi wa Kisesa na eneo la Kanyama kuwa watulivu na
hakuna haja ya kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kukamatwa na Polisi.
"Napenda kuwaeleza wananchi kuwa vyombo
vya dola havitawakamata hovyo wananchi hao na wanaokimbia ni wale
wanaodhaniwa ni waliotekeleza unyama na kutaka kuwa watulivu na
kuisaidia serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwakamata
watu waliohusika na si vinginevyo.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi punde
baada ya kuwasili kwa kijana mkubwa wa marehemu kutoka nchini Uingereza
zimeeleza kuwa huenda mazishi ya mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM mkoa
wa Mwanza, Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Magu, Mjumbe wa Bodi
ya NCU 1984 Ltd, Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA, Mjumbe wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa (NEC), Mdau wa sekta ya Kilimo cha Pamba na mazao mengine
ya chakula, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na aliyekuwa Diwani wa
Kata ya Kisesa hadi mauti yanamkuta yanatarajiwa kufanyika siku ya
Alhamisi juma hili.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho na
kuhudhuria mazishi ya mama yake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Melick
Sadiki aliyefariki leo sanjari na msiba huo wa mwenyekiti wa zamani
ambaye alimuongoza kuomba kura kwa wananchi wa Mkoa huu katika Wilaya 7
katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 akiwa Mwenyekiti wa CCM
kabla ya kushindwa uchaguzi wa CCM mwaka jana (2012) na mwenyekiti wa
sasa Dkt. Anthony Dialo.
Chanzo: GSENGO BLOG
0 comments:
Post a Comment