LATEST POSTS

Tuesday, December 17, 2013

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA YATENGA HEKTA 14 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI

HALMASHAURI ya Manispaa Tabora inatarajia kutenga jumla ya hekta 14 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Alfred Luanda kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya hiyo (DCC) kilichoketi kwenye ukumbi wa manispaa hiyo.
Luanda alisema awali manispaa ilitenga eneo la ujenzi wa hospitali hiyo karibu na kambi ya Wachina, lakini kiwanja hicho kilikuwa hekta 6.2 huku ramani iliyotoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inahitaji kuwa na hekta 12.
Alisema waliamua kukaa kama menejimenti ili kuomba eneo la Shule ya Sekondari Wasichana Tabora kwa kuwa kuna eneo lenye ukubwa wa hekta 97.
Luanda alisema baada ya kutembelea na kuliona eneo hilo, waliomba hekta 14 hasa kwa kuzingatia baadhi ya wavamizi wameanza kuingia katika eneo hilo.
“Kutokana na mchakato huo, hakuna ofisi yoyote waliyokwenda kupata ushauri wa maamuzi hayo na ndipo kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya waliafikiana suala hilo,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kikao cha Baraza la Madiwani pamoja na cha Bodi ya Shule ya Sekondari wasichana Tabora waliunga mkono hatua ya kumega eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments: