Moja ya basi litakalotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT)
likitoka katika kituo cha Ubungo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa
madereva watakao toa huduma za usafiri katika mradi huo, Dar es Salaam
jana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia amezindua rasmi mafunzo maalumu ya
madereva wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), mradi unaotekelezwa jijini
hapa.
Uzinduzi wa mafunzo hayo ni ishara ya kukamilika
kwa awamu ya kwanza ya mradi wa DART wenye urefu wa kilomita 20.9 kutoka
Kimara hadi Kivukoni. Mabasi ya majaribio na wakufunzi kutoka China
wameshawasili kuwajengea uwezo madereva wa ndani.
Ghasia alisema mradi huo ni kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na wa pili Afrika baada ya ya Afrika Kusini.
“Kutakuwa
na mfumo wa kuratibu mabasi yote yaliyo barabarani ili kuona mienendo
na kama kutakuwa na jambo lolote lisilo la kawaida vyombo vya usalama
vitachukua hatua mara moja. Matendo ya dereva na abiria pia yataonekana
wazi kupitia mfumo huo,” alisema Ghasia
Jukumu la
mafunzo ya udereva na matengenezo ya magari hayo mapya na ya kisasa
limekabidhiwa kwa Chuo cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Chuo cha Mafunzo
ya Ufundi Stadi (Veta).
Katika safari moja ya
majaribio kutoka Ubungo hadi Kimara; kwenda na kurudi, basi moja refu
lilitumia dakika 14 likiwa limewabeba Waziri Ghasia; Mkuu wa Mkoa wa
Dar, Said Mecky Sadiki; makamanda wa polisi, Suleiman Kova na Mohammed
Mpinga na baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment