Habari
zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia
baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la
Isuna mkoani humo.
Habari
zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo
namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki
walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.
chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment