STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Jacqueline Wolper akiwa na mchumba wake wa sasa G. Modo.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa
kimya kwa muda mrefu kwa ajili ya kutafakari kwanza maana asingeweza
kukurupuka wakati bado hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake
huyo.
“Kiukweli nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja
kwa moja kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na
Mungu, ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi
niliyempata ni sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Wolper
aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu
kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja kwa wazazi wa pande zote mbili
ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.
0 comments:
Post a Comment