HUU
ni ukatili uliopitiliza! Wakati wanaharakati mbalimbali nchini
wakiwemo wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) wakipinga vikali vitendo
vya ukatili, baba wa kufikia, Musa Mdetela, mkazi wa mjini hapa
anasakwa na polisi kwa kosa la kuwachoma moto miguuni wanaye wa kambo.
Mtoto aliyechomwa na moto sehemu za miguu na baba yake wa kambo.
Mdetela anadaiwa kuwafanyia unyama huo watoto hao, Baraka anayesoma
darasa la kwanza na Mudi wa darasa la sita baada ya kuwatuhumu kuwa,
waliiba shilingi 10,000.
Wakizungumza na mwandishi wetu wakiwa katika sura ya huzuni, watoto
hao walisema baba huyo aliwatendea unyama huo Januari 3, mwaka huu
ambapo walijitetea kuwa walichukua ‘teni’ hiyo kwa ajili ya kununulia
msosi baada ya mama yao kushindwa kuwaandalia chakula.
Hata
hivyo, Mudi alisema siku ya tukio mdogo wake (Baraka) aliingia
chumbani kwa baba yao na kuchukua kiasi hicho cha fedha kisha
wakashirikiana katika matumizi ambapo walinunua bagia na vitumbua ili
wajipoze kwa njaa.
Wakizungumzia kuhusu baba yao mzazi (jina tunalo), walisema aliwaacha
mkoani hapa kwa muda mrefu na sasa anaishi jijini Dar es Salaam hivyo
wao wamebaki na baba mdogo huyo ambaye mara kwa mara amekuwa
akiwaadhibu vikali na kuwanyima chakula.
Kwa
masikitiko makubwa, walisema baada ya baba yao kurudi kutoka kwenye
shughuli zake na kubaini katika akiba yake teni haipo ndipo
alipowakamata na kuwafunga kamba na kuanza kuwatesa kwa kichapo ili
waseme mtu aliyekwapua pesa hiyo.
“Alitufunga kamba miguuni na mikononi na kuanza kututesa kwa
kutupiga. Alipoona hatusemi, akachukua manailoni na kutufunga miguuni
kisha akachukua kiberiti na mafuta ya taa na kuwasha moto miguuni kwetu.
“Tulilia
sana, akaendelea kutupiga na moto ukiwaka. Wakati huo mama alikuwa
amekaa mlangoni akishangilia na kusema wapige sana mimi nimewachoka hao
watoto, heri wafe tu,” walisema watoto hao.
Imedaiwa kuwa baada ya kutekeleza unyama huo, baba huyo aliwafungia
ndani watoto hao na kuwaambia wasitoke nje ndipo majirani walioshuhudia
tukio hilo walipotoa taarifa polisi katika kitengo cha dawati la jinsia
wakalivalia njuga swala hilo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Iringa, Atupele Mwambunda
alizungumza na mwandishi wetu na kusema wamefanikiwa kumkamata mama wa
watoto hao, Watende Sanga huku mumewe, Mdetele aliyekimbia akitafutwa
kwa udi na uvumba ili kufikishwa kwenye mikono ya sheria.
Akiwa katika ofisi za dawati la jinsia, mama wa watoto hao alidai
wakati baba yao mdogo akiwapa mbata watoto hao yeye hakujua
kinachoendelea japokuwa alipata taarifa ya kupotea kwa pesa.
Aliendelea kusema kuwa, baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa watoto
hao ili kuwatibu kinyemela pamoja na kuwaombea ruhusa shuleni.
Mwanamke huyo aliomba kusamehewa kwa vile hakujua kama kushangilia wakati baba yao akiwapa adhabu watoto hao ni kosa. Anaendelea kushikiliwa na polisi mkoani hapa.
Mwanamke huyo aliomba kusamehewa kwa vile hakujua kama kushangilia wakati baba yao akiwapa adhabu watoto hao ni kosa. Anaendelea kushikiliwa na polisi mkoani hapa.
Chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment