LATEST POSTS

Saturday, January 18, 2014

Mkenya ateuliwa kuwania tuzo za Oscar

Orodha ya walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar, imetolewa.
Mkenya wa kwanza kuwahi kuwa katika Orodha hiyo pia ametajwa.
Si Mwingine bali ni Lupita Nyong'o nyota wa filamu liyowagusa wengi yenye mada utumwa, 12 years a Slave'.

Lupita mwenye umri wa miaka 30 amepata uteuzi wa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi katika filamu za mwaka 2013.
Atamenyana na magwiji wa uigizaji Julia Roberts na Jennifer Lawrence katika tamasha la tuzo za Oscars mwaka 2014.
Babake Lupita ambaye ni mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya ameelezea kufurahishwa sana na taarifa hizo na kumtakia kila la heri binti yake.
Kwenye filamu ya '12 years a Slave', Lupita aliigiza kama mtumwa aliyetumiwa kama mtumwa wa kingono na mkubwa wake.
Tangu filamu hiyo iliyotengezwa mwaka 20131, kutolewa, nyota ya Lupita imekuwa iking'aa kwani amejipata akiwa katika kumbi moja na wagizaji maarufu kama Brad Pitt, Julia Roberts na wengineo hali ambayo kwa wengi itasalia kuwa ndoto.
Alipata uteuzi katika tuzo za Golden Globes za Uingereza ingawa hakuweza kushinda .

Chanzo: BBC Swahili

0 comments: