ESTER CHARLES (16) ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Rebu iliyoko wilayani Tarime mkoani Mara, alishindwa kujizuia na
kudondosha machozi katika ukumbi wa kantini ya jeshi la polisi wilayani Tarime
baada ya kueleza masaibu aliyokumbana nayo kwa kufanyiwa ukeketaji na wazazi
wake.
Anapofanyiwa ukeketaji
huaminika kuwa mwanamke kamili aliyeondolewa mkosi na ambaye anastahili kuolewa.
Wakati anafanyiwa ukatili huo, Esta alikuwa anasoma darasa la saba katika shule
ya msingi Rebu, ambapo mara baada ya kukeketwa, anasema alipata maumivu makali
ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi.
Anasema alikubali kufanyiwa
ukeketaji na wazazi wake baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na alikuwa
na hamu ya kuendelea na masomo, lakini akapewa masharti na wazazi wake kuwa ili
aendelee na masomo lazima akeketwe.
“Sikuwa na jinsi, nilijua
ningeenda kukumbana na maumivu makali na kwasababu nilikuwa napenda shule
ilinibidi kukeketwa” anaeleza.
UKEKETAJI
UNAFANYIKAJE?
Anasema aliamshwa saa 11:30
alfajiri akiongozana na mama
yake na wanawake wengine watatu alikwenda kuungana na wasichana wenzake
waliokuwa kwenye orodha ya kufanyiwa ukeketaji na kupelekwa mtoni
kuogeshwa!
Tuliogeshwa na kupewa maneno
ya ujasiri ili tusilie wakati wa kukeketwa “ anasema na kuongeza kuwa Ngariba
alilipwa kiasi cha Sh. 10,000/= kwa kila msichana aliyekeketwa (kwa wakati huo).
Esta anasema kuna eneo maalum lililotengwa kwaajili ya shughuli hiyo na msichana
hushikwa mikono yake kwa nyuma na mama aliyekeketwa.
“Baada ya kufika eneo lile,
tulitangaziwa na ngariba kuwa kila mmoja awe na wembe wake, ambao ndiyo alitumia
kukeketa” anasema.
Anachokumbuka siku hiyo ni
kujikuta tayari amekwisha keketwa huku akitokwa na damu nyingi na maumivu
makali. Anasema baada ya kukeketwa, wasichana wote waliwekwa katika uangalizi wa
akina mama wasaidizi wakiwemo baadhi ya ngariba, huku wakiwapatia dawa za
kienyeji wale wanaovuja damu iliisiedelee kuvuja.
Nilishindwa kula,
nilikunywa uji tu, siku ya pili nilipata maumivu makali baada ya kuamshwa
asubuhi kwenda kuogeshwa” anaeleza.
Wakisikiliza kwa makini ni washiriki wa Kongamano hilo lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuibua changamoto zilizopo katika jamii kuhusu suala la ukeketaji |
Anasema msichana anapotoka
jandoni inambidi ashiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye amefanyiwa tohara
kama ishara ya kukubali kuwa binti aliyekeketwa kuwa mwanamke kamili na
anayestahili kuolewa. Msichana aliyekeketwa huitwa ‘Omonke’.
Anaiomba serikali, asasi za
kiraia na waandishi wa habari kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa
kike, na kwa ngariba wapewe elimu ya kutosha dhidi ya madhara ya
ukeketaji.
“Wengi huku Tarime wanafanya
hivyo, wakijivunia kukeketwa kutekeleza mila lakini pia ngariba bado hawajapata
elimu ya madhara ya ukeketaji, naiomba serikalia na wadau wengine watoe elimu
zaidi juu ya madhara ya ukeketaji” anasema na kuongeza kuwa jamii yao huamini
kuwa wakimkeketa motto wa kike huleta Baraka katika familia.
NI MADHARA GANI ALIYOKUMBANA
NAYO?
Anasema baada ya kukeketwa
aliumia sana na aliathirika kisaikolojia ikiwemo kuzomewa nna wasichana wa rika
yake ambao hawakuwa tayari kukeketwa.
“Siku niliyokeketwa,
nilipata shida sana, nilikuwa na hofu hata wenzangu walikuwa wakinicheka, hata
nilipopona nilichukua muda kurudi shule, niliathirika sana” anasema madhara
mengine aliyo yapata ni pamoja na kuchanika sehemu zake za siri, kutokana na
kukeketwa akiwa na wasiwasi kama atajifungua salama siku za
baadaye.
“Mimi nahisi hata wakati wa
kujifungua, nitapata matatizo, naomba wazazi wetu wabadilike waanze kwenda na
wakati na watambue kuwa wanapotufanyia ukeketaji wanatufanyia ukatili wa
kijinsia na kilema cha maisha” anasema.
Anasema kuwa kuna uwezekano
wa wasichana wanaokeketwa kupata virusi vya ukimwi kutokana na kukeketwa ba
ngariba mmoja, ambaye hukeketa zaidi ya wasichana 50 kwa siku.
Ester anaahidi kuhakikisha
wadogo zake Neema na Happy kuwa hawato keketwa kwani yeye kashakuwa mkubwa
anayejitambua ana kujua kujieleza.
NDOTO ZA BAADAYE ZA
ESTA.
“Nitasomea uandishi wa
habari, nitafanya kazi kwa bidii na natamani niwe kama Waziri wa Maendeleo ya
Wanawake, Jinsia na Watoto, Sophia Simba. Nampenda jinsi anavyo wahudumia
wanawake” anasema. Ameiomba serikali kupitia
jeshi la polisi kuwakamata mangariba wote wanao husika kufanikisha ukeketaji na
kuwafikisha mahakamani, ili sheria ichukuemkondo wake .
Anaitaka jamii ya Wakurya
kuendeleza watoto wa kike kitaaluma zaidi badala ya kuwaoza wakiwa katika umri
mdogo, na hivyo kushindwa kuhilili kutunza familia.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu ya Tarime – Rorya, Emmanuel Mkoma anasema kuwa jeshi la polisi kwa
kushirikiana na wadau wengine wilayani Tarime, limeanza kutoa mafunzo ya tohara
mbadala itakayo iwezesha jamii kutambua athari za ukeketaji kwa watoto wa
kike.
Hisia za mmoja kati ya wanafunzi wa kiume na uelewa wa suala la ukatili wa kijinsia na ukeketaji wilayani Tarime mkoani Mara. |
Lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa jamii,
ambapo watoto wa kike watapewa elimu ya malezi ya Afya zao itakayo wasaidia
wasikeketwe, msisitizo wake ni kuelimisha jamii ione madhara ya ukeketaji na
kadri siku zitakavyo kwenda jeshi la polisi linaimani kuwa jamii itaachana na
ukeketaji.
Chanzo: Gsengo
0 comments:
Post a Comment