Mada ya wiki
Makala hii inatoa maelekezo kuhusu ulishaji wa
mtoto wakati mama hana
virusi vya UKIMWI, hajui hali yake ya
uambukizo na pia wakati mama anaishi na
virusi vya UKIMWI.
Elimu kuhusu ulishaji watoto katika hali ya
kawaida ni msingi
muhimu kwa mama kuelewa
jinsi ya kumlisha mtoto wakati ana virusi vya UKIMWI.
Pia, makala hii haitoshi kumfanya mlishaji wa
mtoto kuwa na stadi na utaalamu wa
kutosha kwenye eneo hilo.
Ili kuweza kutoa huduma kamilifu kwa hili mama
anayeishi na
virusi vya UKIMWI kuhusu kumlisha mtoto,
anahitaji mafunzo zaidi
Taarifa
ambazo nimeziweka kwenye makala hii ni kumwezesha mama husika
kupata mwanga au kuelewa kwa kiasi jinsi ya
ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama
anayeishi na virusi vya
UKIMWI.
Kwa wanawake ambao hawana virusi vya UKIMWI,
wale ambao hawajui hali zao za
uambukizo na wale waliopima lakini
hawakuchukua majibu; wote wanakuwa katika
kundi moja; ambapo hushauriwa kumlisha mtoto
kama kawaida na kufuata taratibu za
kawaida za kunyonyesha.
Maziwa ya mama ndiyo chakula pekee na bora
zaidi kwa mtoto mchanga kuliko
maziwa mengine yoyote. Kugundulika uwezekano
wa maziwa ya mama
kumwambukiza mtoto virusi vya UKIMWI kumesababisha
wataalamu kushauri
utumiaji wa maziwa mbadala au kurekebisha
namna ya kunyonyesha ili kupunguza
uwezekano wa uambukizo wa virusi vya UKIMWI
kwa mtoto. Ni muhimu
ikumbukwe kuwa chakula
cha mtoto chini ya umri wa miezi sita ni maziwa pekee.
Ulishaji
wa mtoto wakati mama hana virusi vya UKIMWI au
hafahamu
hali yake ya uambukizo
Kunyonyesha maziwa ya
mama
Ni dhahiri kuwa maziwa ya mama ndiyo lishe
bora kwa mtoto mchanga kuliko maziwa
mengine yoyote. Kunyonyesha maziwa ya mama
kunampa mama pamoja na mtoto
faida nyingi.
• Faida
kwa mtoto:
·
Humpatia virutubishi vyote anavyohitaji kwa uwiano ulio sahihi
kwa ukuaji wa akili na mwili kwa miezi sita ya mwanzo;
·
Humpatia kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kama kuharisha,
maradhi ya njia ya hewa na masikio;
·
Huleta uhusiano mzuri na wa karibu kati ya mtoto na mama;
·
Watoto walionyonya maziwa ya mama huwa na mwenendo mzuri pamoja
na akili zaidi ukilinganisha na wale wasionyonya maziwa ya mama.
·
Maziwa ya mama huyeyushwa kwa urahisi tumboni mwa mtoto na hivyo
kusharabiwa na kutumiwa na mwili kwa ufanisi.
· Faida kwa mama:
· Mama anaponyonyesha mara baada ya kujifungua husaidia tumbo la
uzazi kurudi katika hali ya kawaida mapema. Pia husaidia kupunguza damu kutoka
baada ya kujifungua hivyo huchangia kuzuia upungufu wa wekundu wa damu;
· Hupunguza uwezekano wa kupata ujauzito katika miezi sita ya
mwanzo kama mama atamnyonyesha mtoto maziwa yake pekee mara nyingi (zaidi ya
mara 10) kwa siku na pia kama hajapata hedhi katika miezi sita ya mwanzo;
· Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi na
matiti;
· Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto; na
· Iwapo mama aliongezeka uzito mkubwa wakati wa mimba, kunyonyesha
husaidia kumrudishia mama umbile lake la kawaida.
Faida nyingine za maziwa ya mama:
·
Ni safi, salama na
hupatikana muda wote katika joto sahihi kwa mtoto na hayahitaji matayarisho;
·
Hayaharibiki ndani ya
titi na hata yakikamuliwa huweza kukaa kwa muda wa saa 8 katika joto la kawaida
bila kuharibika, na saa 72 kwenye jokofu;
·
Gharama yake ni ndogo ukilinganisha
na maziwa mbadala;
·
Nchi huokoa fedha za kigeni ambazo
zingenunulia maziwa mbadala na dawa;
·
Huokoa muda wa mama na
fedha za familia ambazo zingenunua maziwa mbadala au kulipia matibabu;
·
Hayaleti matatizo ya mzio
(allergies) kama pumu na magonjwa ya ngozi;
· Kunyonyesha maziwa ya
mama huchangia kutunza mazingira, kwani hayaachi mabaki kama makopo na chupa
ambavyo hutumika kwa maziwa mbadala;
· Maziwa ya mama yana maji
ya kutosha hivyo mtoto chini ya miezi sita hahitaji maji;
Mapendekezo ya kumsaidia mama ili anyonyeshe kwa ufanisi
·
Mtoto aanze kunyonya maziwa ya mama mara tu baada ya kuzaliwa
(katika saa
moja ya mwanzo);
·
Mama aliyejifungua kwa operesheni, asaidiwe ili aanze
kunyonyesha mara
anapopata fahamu. Inaweza
kuchukua hadi saa sita kupata fahamu, mtoto
asipewe maji ya sukari au
ya kawaida. Mama ambaye hakupewa dawa ya usingizi anaweza kuanza kunyonyesha
mapema zaidi;
· Mtoto anyonyeshwe kila
anapohitaji usiku na mchana ili kuendeleza utokaji mzuri wa maziwa ya mama;
· Mtoto asipewe kitu kingine
chochote hata maji, isipokuwa maziwa ya mama mpaka afikie umri wa miezi sita;
·
Mtoto apakatwe kwa namna
ambayo anafikia titi vizuri.
·
Wakati wa kunyonyesha,
chuchu yote na sehemu kubwa ya eneo jeusi linalozunguka chuchu liingie kinywani
kwa mtoto.
·
Mtoto afikishapo umri wa
miezi sita inashauriwa kuanza kumpa chakula cha
·
nyongeza huku akiendelea
kunyonya maziwa ya mama. Mtoto apewe chakula cha nyongeza kwa kutumia kikombe
au kibakuli na kijiko;
· Mtoto anyonyeshwe kwanza,
ndipo apewe chakula cha nyongeza (baada ya miezi 6);
·
Vyakula vya nyongeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi
yafuatayo ya vyakula:
Vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi
· Vyakula vinavyotokana na
wanyama na jamii ya mikunde
· Mboga-mboga
· Matunda
· Mafuta na sukari (kwa
kiasi)
Mtoto aendelee kunyonya mpaka afikie umri wa
miaka miwili au zaidi, huku akipewa chakula mara tano au zaidi kwa siku;
Jinsi ya kumpakata na kumweka mtoto kwenye titi
Picha 1
(a)
inaonyesha
njia sahihi ya kumshika mtoto ili afikie titi vizuri. Tumbo la mtoto limemwelekea mama na uso
umeangalia na umesogelea titi.
Picha 1
(b) inaonyesha njia
ambayo
si sahihi ya kumshika mtoto. Hapo mtoto hataweza kuingiza titi kinywani
vizuri.
Picha 2
(a) inaonyesha mtoto ambaye titi limeingia vizuri kinywani yaani chuchu pamoja
na sehemu
nyeusi inayozunguka chuchu imeingia kinywani. Midomo iko wazi na kidevu kimegusa titi. Mtoto
atanyonya vizuri.
Picha
2. (b) inaonyesha mtoto ambaye hakuingiza titi vizuri kinywani. Mtoto huyu
ananyonya chuchu tu, midomo haikufunguka vizuri na kidevu kiko mbali
na titi. Mtoto hataweza kunyonya vizuri.
MUHIMU
Mtoto anayepewa chakula cha nyongeza, ni
vyema anyonyeshwe
kabla ya kulishwa.
1 comments:
Ukweli i ilijaribiwa HIV + chanya miaka 3 iliyopita. Mimi kuendelea kusimamia madawa ya kulevya i kawaida kununua na huduma za shirika la kuweka mimi afya na kuimarisha , i walijaribu kila i unaweza pia kufanya ugonjwa huu kuniacha peke yake, lakini kwa bahati mbaya ni kuweka juu ya kula me up hii ni nini i unasababishwa yangu, kwa kuruhusu kufanya ngono yangu mkweli kwangu insecurely bila ulinzi, ingawa i kamwe alijua yeye ni virusi vya UKIMWI. Hivyo michache iliyopita siku 4 i alikuja katika kuwasiliana na makala ya kusisimua kwenye mtandao juu ya jinsi hii Nguvu Herb Mganga kupata vizuri yake na kupona. Hivyo kama mgonjwa i anajua matakwa ya hii alichukua maisha yangu siku 1, na i haja ya kuishi na marafiki na jamaa wengine pia. Hivyo i kunakiliwa nje Dk PAUL waganga wa jadi ya kupitia barua pepe: okonofua_solution_tem99@hotmail.com na mimi barua pepe naye mara moja , katika kidogo wakati yeye mail yangu nyuma kwamba i alikuwa kuwakaribisha kwa Hekalu lake nyumbani walikuwa na yote yale i kutafuta kwa ni nafasi . Mimi nilikuwa tafadhali wakati huo. Na i kuendelea naye, alichukua baadhi ya maelezo chache kutoka kwangu na aliniambia kuwa yeye atakuwa kupata nyuma kwa haraka kama yeye ni kupitia kwa kazi yangu. Mimi nilikuwa na furaha sana kusikia kutoka kwake . Hivyo Jana, kama i mara tu kuja kutoka nyumba marafiki zangu , Dk EMEN kuniita kwenda kwa checkup katika hospitali na kuona kazi yake ya ajabu kwamba ni sasa VVU, i ilikuwa furaha sana kusikia kutoka kwake , hivyo i haraka kukimbilia chini ya hospitali karibu na kupatikana nje, tu kusikia kutoka daktari wangu hospitali aitwaye HARRISON kwamba mimi sasa VVU. Mimi kuruka hadi saa yake na mtihani kumbuka, yeye kuuliza jinsi gani kutokea na i kupungua kwa yake yote i akaenda kupitia kwa Dr Paul EMEN sasa niko furaha , hivyo i ni aina ya upole wa mtu kwamba haja ya kushiriki ushahidi huu kila mtu ambaye kutafuta kwa ajili ya uponyaji , kwa sababu mara moja kupata utulivu na utulivu, hivyo ugonjwa kupata kumaliza maisha yako mbali. Hivyo i atakushauri kuwasiliana naye Leo kwa ajili ya uponyaji wako katika maelezo ya hapo juu : Email ID: okonofua_solution_tem99@hotmail.com kuwasiliana naye sasa kuokoa maisha yako kama unataka kuuliza swali lolote email yangu: aminahkadiri@gmail.com i nimefurahi hivyo kujibu yoyote ya mwili katika sanamu zangu rasmi. ndio tena shukrani kwa DR PAUL EMEN kwa kuwa ni nguvu na msaada.
Post a Comment