HALI ya afya ya mtoto
wa kike mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la nne, shule ya
msingi Bwanza, kata ya Kisorya, wilaya ya Bunda mkoani Mara, aliyeingiwa
na samaki sehemu zake za siri na kukimbilia tumboni inazidi kuimarika.
Mtoto huyo ametoa ushuhuda wa tukio hilo akisema hatalisahau kamwe maishani mwake.
"Nilikuwa
nateka maji ziwani, samaki huyo aina ya sato akarukia miguuni mwangu,
akaingia sehemu za siri na kukimbilia tumboni, nilijaribu kumvuta lakini
sikufanikiwa, kwani alizama kabisa tumboni kupitia sehemu zangu za
siri," alisema mtoto huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.
Mtoto huyo
anayetibiwa kwa mganga wa jadi aliyejitambulisha kwa jina moja la
Mshaki alisema, samaki huyo alipomuingia sehemu zake za siri, alisikia
maumivu makali na kushangaa namna samaki huyo alivyokua akiteleza
kuingia tumboni.
Alisema kila alipokuwa akijaribu kumvuta ili amtoe, alihisi maumivu makali zaidi hivyo akalazimika kumwacha na kuingia tumboni.
"Samaki
alipoingia huku chini miguuni na kukimbilia tumboni, niliishiwa nguvu,
nilimuita dada Monica niliyekuwa naye ziwani akanisaidia kunishika hadi
nyumbani, usiku sikulala, tumbo lilikuwa likiniuma mno, kila
nilipojisaidia haja ndogo nilikuwa nikijichungulia na kuona mkia wa
samaki huyo ukitokea, hata bibi Emakulata naye alimwona
aliponichungulia," alisema mtoto huyo.
Alisema kwa sasa anaendelea
vizuri baada ya kutibiwa na mganga huyo wa kienyeji mkazi wa kijiji cha
Amuyebe, Ukerewe mkoani Mwanza japo alisema baada ya kupewa dawa,
alitokwa na harufu mbaya.
Aidha, mganga huyo wa jadi, akizungumza na
Majira kwa njia ya simu. alikiri kumtibu mtoto huyo akidai alichezewa
kichawi kwa kuingiziwa dawa tumboni kupitia sehemu zake za siri kwa
mwonekano wa samaki, dawa ambayo alisema, ilikuwa iozeshe viungo vyote
tumboni na kumsababishia kifo.
"Mtoto huyu alirushiwa kombora katika
mwonekano wa samaki aliyeingia tumboni mwake kupitia sehemu zake za
siri, lengo likiwa ni kumuua baada ya kuozesha viungo vyote tumboni
lakini, nimemwahi kabla hajaharibu tumbo lake kwa kumpa dawa ya kumfanya
aharishe na kukojoa mara kwa mara, ndiyo maana alitokwa na harufu
mbaya.
Bibi wa mtoto huyo, Emakulata Mtani (64), alisema ana furaha
kubwa kutokana na maendeleo mazuri ya afya ya mjukuu wake akiamini kwa
hali ilivyo sasa atapona.
Januari mosi, mwaka huu mtoto huyo akiwa
anateka maji katika Ziwa Victoria kumwagilia bustani ya nyanya na
vitunguu, alidai kurukiwa na samaki aina ya sato sehemu zake za siri,
aliyepenya hadi tumboni mwake.
Miongoni mwa viongozi waliozungumza
na Majira na kuthibitisha kupata taarifa za kutokea kwa tukio hilo la
aina yake ni mwenyekiti wa kitongoji cha Alwego Leticia Bituro, Diwani
wa kata ya Napindi Elias Magoti, Kamanda wa Jeshi la Polisi wilaya ya
Bunda (OCD) Mika Nyange.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment