LATEST POSTS

Wednesday, February 26, 2014

Halmashauri yaagizwa kutengeneza Magari yake

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imeagizwa kutengeneza Magari yake ili 

watumishi waanze kwenda kwa wananchi Vijijini.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mh.John 

Kadutu,alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo Mjini Kaliua.

Amesema watumishi kipindi hiki hawawezi kwenda kwa wananchi kusikiliza na 

kutatua kero zao kutokana na ukosefu wa magari ambayo ni mabovu na kuaagiza 

magari yote mabovu yawe yametengenezwa katika kipindi kisichozidi wiki mbili 

kuanzia sasa.

Mwenyekiti huyo ametaka watumishi wote kufanya kazi zao kwa malengo na sio 

kufanya kazi kwa mazoea na kwamba wanatakiwa kueleza wamefanya mambo 

gani katika kipindi walichojipangia

Kwa upande wa mapato,Kadutu ameagiza kila Mkuu wa Idara awe katika nafasi 

ya kueleza jitihada alizofanya katika kukusanya mapato ya halmashauri kwenye 

Idara yake.

Amesema wakati umefika wa Halmashauri kuzidi kupanua wigo wa ukusanyaji 

mapato na sio kutegemea ushuru wa zao la Tumbaku peke yake.

Halmashauri ya wilaya ya Kaliua imeanzishwa baada ya kugawanywa 

Halmashauri ya wilaya ya Urambo ambayo inategemea zaidi ushuru wa zao la 

tumbaku ambalo ndio zao kuu la Biashara.

0 comments: