LATEST POSTS

Friday, February 7, 2014

Lulu kusomewa mashtaka February, 17 mwaka huu

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba atasomewa mashtaka yake Februari 17, mwaka huu.
Lulu atasomewa mashtaka yake mbele ya Jaji Rose Teemba wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ambapo siku hiyo atatakiwa kujibu kama kweli au si kweli.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na vikao vya mahakama, Lulu baada ya kusomewa mashtaka kesi hiyo itapangwa terehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali, kabla ya kuanza kusikilizwa rasmi.
Lulu anatuhumiwa kumuua Kanumba, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu, Sinza, Dar es Salaam.

 

Elizabeth Michael

0 comments: