wadau mbalimbali |
Wadau wa filamu |
Uzinduzi
huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya filamu hapa nchini
pamoja na mashirika ya ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni hatua ya kuleta
mapinduzi makubwa katika sekta ya filamu hapa nchini.
Filamu
zilizozinduliwa jana zikiwa na lengo la kuelimisha jamii ni Mdundiko
iliyotengenezwa na Timothy Conrad, Sunshine iliyotengenezwa na Karabani
na Network iliyotengenezwa na John Kallage.
Mradi
wa Swahiliwood umewezeshwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia USAID
kwa kushirikiana na Johns Hopkins University Center for Communication
Programs pamoja na kampuni ya Proin Promotion inayokuwa kwa kasi katika
usambazaji wa kazi za filamu nchini Tanzania.
Lengo
la Swahiliwood ni kuongeza nguvu ya ubunifu kwa vijana watengeneza
filamu wa Kitanzania, ili kupeleka maudhui kwa walengwa kwa njia ya
burudani kwa kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha filamu
zinawafikia walengwa mbalimbali kupitia mitandao ya wasambazaji. Mradi
huu unafanya kazi pamoja kwa kushirikiana na wadau muhimu kutoka sekta
ya umma pamoja na COSOTA (Chama cha haki miliki), Mamlaka ya mapato
Tanzania, bodi ya filamu na BASATA, kama idara inayosimamia maendeleo ya
Tasnia vya filamu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi John Riber, mkurugenzi MFDI Tanzania alisema kwamba
“Tulizindua mradi wa Swahiliwood kwa sababu tuliona kwamba vijana wana
uwezo mkubwa wa kutengeneza filamu. Muundo wa Swahiliwood unazingatia
nguvu ya vijana katika kuhakikisha tasnia ya filamu inasambaa
ikielimisha jamii juu ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Na hiyo
imetambuliwa na Serikali ya Tanzania kama ni changamoto kuu ambayo
inalikabili Taifa”.
Muundo
wa Swahiliwood unatoa mafunzo na ushauri kwenye uzalishaji wa filamu.
Pia ni sekta ambayo inaongoza kwa kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania.
Serikali ya Tanzania na sekta binafsi pamoja na Watanzania wabunifu
wenye vipaji vya utengenezaji wa filamu wameshirikiana, kwa msaada wa
Serikali ya Marekani. Wamekuwa nyenzo katika kukuza biashara na uchumi
unaokuwa haraka, na kuhakikisha kwamba filamu zinawafikia watazamaji wa
Afrika ya Mashariki kwa ujumla.
MDUNDIKO: Ni hadithi ambayo inazungumzia mfarakano wa imani za kimila, maadili, na hoja za maisha katika jamii.
NETWORK:
Ni hadithi inayohusu kuwindwa kwa mhalifu anae tuhumiwa kufanya mauaji
ya mwendelezo ambayo yanawahusisha wapelelezi, askari mzee na kijana
mwenye mvuto.
SUNSHINE: Ni hadithi ya uraiani yenye mguso kuhusu majaribu ya uhalifu na mapenzi yasiyokuwa na mashariti kati ya mama na mtoto.
0 comments:
Post a Comment