Mtangazaji maarufu Gardner G. Habash akiwa na demu mjamzito.
REVENGE! Katika kile kinachoonekana kama kejeli kwa mke wake
wa zamani aliyekorofishana naye, mtangazaji maarufu Gardner G. Habash,
ametundika picha kwenye akaunti yake katika mtandao wa Instagram
ikimuonyesha akiwa amempakata mwanamke mjamzito.
Gardner, mume wa ndoa wa nyota wa Bongo
Fleva, Judith Wambura Mbibo, anayesadikika kuwa na matatizo ya uzazi,
aliiweka picha hiyo akiificha sura ya mwanamke huyo, lakini akionyesha
kulishika tumbo huku akiachia tabasamu na kusindikizia na maneno kuwa
mambo mazuri yako mbioni kuja.
Katika maoni mbalimbali ya wadau
waliozungumzia suala hilo, baadhi walimpongeza kwa kumpata mwanadada na
kumpa ujauzito, huku wengine wakihoji kama huyo ndiye shemeji au wifi
yao.
Wapo waliokwenda mbali zaidi na kudai
mtangazaji huyo wa zamani wa Times FM, alikuwa amefanya kitendo hicho
makusudi ili aweze kumkejeli Jide, ambaye alikaa naye kwa muda wa miaka
kumi pasipo kupata mtoto.
“Jamani hivyo siyo vizuri maana
anamkejeli tu dada yetu Jide, sijui anaona raha gani kumuumiza mwenzake
moyo,” aliandika mdau mmoja.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Gardner
na kutaka kufahamu kuhusu ukweli wa picha hiyo na kama alikuwa na lengo
la kumkejeli mwandani wake huyo wa zamani.
“Yaa, ni kweli picha nimeweka
mimi..lakini si kwa lengo la kumkejeli Jide, kwa nini nimkejeli? Mimi
sina matatizo naye mbona, ni picha tu nimeweka..
“Huyo ni shemeji yangu, mke wa mdogo
wangu mmoja kifamilia. Lakini usijali, wiki hii nitamwonyesha picha
nzima ili watu wamtambue na nitawaeleza kwa kirefu,” alisema Gardner,
ambaye pia ni mdau mkubwa wa muziki.
Wawili hao waliingia katika mtafaruku
miezi kadhaa iliyopita na tangu wakati huo, hakuna hata mmoja kati yao
aliyeweza kuzungumzia suala hilo moja kwa moja zaidi ya mafumbo
wanayoyatoa kupitia akaunti zao katika mitandao ya kijamii. Jide
hakupatikana kuzungumzia picha hiyo.
0 comments:
Post a Comment