Wasanii mbalimbali wakifuatilia kuhusiana na katiba iliyokataliwa kusikilizwa.
WASANII mbalimbali katika nyanja za sanaa leo wameungana katika ukumbi wa Vijana, Kinondoni katika kuzindua rasmi kampeni ya kuhakikisha mapendekezo yao kikatiba yanasikilizwa na kupitishwa.
Akizindua kampeni hizo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Lebejo Mngereza alisema:
Akizindua kampeni hizo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Lebejo Mngereza alisema:
“Tupo pamoja na wasanii wote, tutahakikisha wasanii wetu wanasikilizwa na kutekelezewa. Haiwezekani msanii kukosa haki zake za msingi kwa muda mrefu.” Alisema.
Awali, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) wakishirikiana na Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) waliandaa na kupeleka mapendekezo mawili yaliofikishwa kwenye Tume ya Katiba. Pamoja na kupokelewa hapakuwepo na jambo lolote lililotokana na mawazo hayo ambalo lilichukuliwa na kuingizwa kwenye Rasimu ya Katiba.
Mapendekezo mawili waliokuwa wameyatoa awali ni pamoja na kutaka wasanii kutambuliwa katika Katiba kama moja ya makundi maalum, kama vile walivyotajwa wavuvi, wakulima, wafugaji na kadhalika.
Pendekezo la pili lilikuwa ni kuweka kipengele cha kulinda na kuendeleza Haki za Miliki Bunifu katika Katiba mpya.
Pendekezo la pili lilikuwa ni kuweka kipengele cha kulinda na kuendeleza Haki za Miliki Bunifu katika Katiba mpya.
0 comments:
Post a Comment