Baba mzazi wa mtoto John akiwa
amekaa na mwanae mara tu baada ya hukumu kutolewa
MWANAMKE Mwanahawa Nassoro(32) Mkazi wa Mtaa wa Airport
jijini Mbeya amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya
kupatikana na hatia ya kunyanyasa na kumtesa mtoto.
Mwanamke huyo alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya
Mbeya mjini juzi kutokana na kosa lililokuwa likimkabili la kumtesa mtoto John
Paul(03) ambaye ni mtoto wa kaka yake.
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo
Mbeya mjini, Salome Mwakyosi, mwendesha mashitaka wa Polisi Kopro Anthon
alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Machi 12, Mwaka huu kwa nyakati tofauti kwa
kumfungia ndani na kumnyima chakula kinyume cha sheria namba 241 ya makosa ya
jinai sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Alisema Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Airport, Rehema
Mohammed ndiye aliyebaini na kutoa taarifa kwenye uongozi wa Mtaa ambapo
mtuhumiwa alikamatwa na hatimaye kufikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya
hutua za kisheria.
Upande wa Mashitaka ulikuwa na mashahidi wane, ambapo
wawili kati yao ndiyo waliotoa ushahidi ambao ni pamoja na Mjumbe wa Serikali
ya Mtaa na Mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye alimtambua mahakamani Shangazi
yake Mwanahawa licha ya kuwepo watu wengi.
Mtoto huyo alifika mahakamani kutoa ushahidi baada ya
afya yake kuimarika kutokana na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya.
Hakimu alipomuuliza mtoto kuhusu mtu aliyekuwa akimpiga
alimuonesha Mwanahawa mara tatu ambapo alizidi kumuonesha Shangaza yake
huyo.
Kwa upande wake mtuhumiwa wa kesi hiyo alipoulizwa
kuhusiana na kosa hilo alikiri ambapo Hakimu aliridhika na ushahidi uliotolewa
na pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kukiri kwa
mtuhumiwa.
Kutokana na ushahidi huo Mahakama hiyo na ilimtia hatiani
mshitakiwa kwa kumuadhibu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe
fundisho kwa watu wanaofanya vitendo vya kikatili dhidi ya
watoto.
Chanzo: Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment