Familia ya afisaa mmoja wa Elimu nchini Kenya imepigwa na
butwaa baada ya kupata jeneza dogo likiwa limewekwa kwenye mlango wao mjini
Kisumu Magharibi mwa Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Taifa Leo, familia ya Afisaa huyo Elias
Oganda, mwenye umri wa miaka 56, ilipata jeneza hilo dogo likiwa na mzoga wa
Paka nje ya mlango wao na sasa inaishi kwa hofu kubwa.
Afisaa huyo anayefanya kazi katika wizara ya elimu, alisema kuwa hii ni mara
ya nne katika miezi sita kupata jeneza kama hilo nyumbani kwake.
Polisi walifungua jeneza hilo na kupata mzoga wa Paka ndani yake. Walishuku
kuwa Paka huyo alinyongwa na kuwekwa ndani ya jeneza hilo kwani hapakuwa na
dalili yoyote ya damu.
Bwana Oganda naye alisema kuwa jeneza hilo liligunduliwa na mkewe Joyce
Oganda, mwenye umri wa miaka 50, usiku wa manane alipotoka nje kujisaidia.
''Nia ya mtu aliyefanya kitendo hicho haijulikani, mimi sijawahi kuhusika na
mzozo wa ardhi'' alisema bwana Oganda aliyeongeza kuwa familia yake haijwahi
kupata utulivu kwa mwaka mmoja uliopita kwani amekuwa akifanyiwa uchawi mara kwa
mara.''
''Hii ni ardhi ya babangu na sielewi kwa nini watu wanataka kunitishia maisha
kwa kutumia uchawi.''
Wakazi walikita kambi katika nyumba ya bwana Oganda kushuhudia mchawi
aliyeletwa katika nyumba hiyo kutoka Sirare mpakani mwa Kenya na Tanzania
kujaribu kujua ni nani aliyehusika na kitendo hicho.
0 comments:
Post a Comment