LATEST POSTS

Wednesday, March 19, 2014

Babu ashikiliwa polisi akidaiwa kumbaka mjukuu wake

MTOTO anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mkata, mkoani Pwani mwenye umri wa miaka saba (jina tunalihifadhi), anadaiwa kubakwa na babu yake mwenye umri wa miaka 42.
Kitendo hicho kinadaiwa kumsababishia maumivu makali na kutokwa damu nyingi wakati akiwa darasani na wenzake ambao walikwenda kutoa taarifa kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Moses Kimlayi, aliyekwenda kushuhudia tukio hilo.
Baada ya kumuona mwanafunzi huyo, Bw. Kimlayi alimkabidhi mwanafunzi huyo kwa walimu wanawake waweze kumchunguza kama amebakwa kutokana na maelezo ya mwanafunzi huyo aliyedai babu yake alimfanyia kitendo hicho na kumtaka asimwambia mtu yeyote.
Hata hivyo, walimu hao walimchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka Kituo cha Polisi Mkata aweze kupewa fomu ya PF3 ambayo itamwezesha kwenda kufanyiwa uchunguzi kwenye Kituo cha Afya Mkata na kupatiwa matibabu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Daktari wa kituo hicho aliyefahamika kwa jina mola la Dkt. Malale, alidai kumpokea mtoto huyo jana saa nne asubuhi kutoka kwa walimu wake.
"Baada ya kumpima, tumebaini mtoto huyu aliingiliwa sehemu za siri, kupata maumivu makali na kutokwa damu hivyo tumempa matibabu," alisema Dkt. Malale na kuongeza kuwa, hilo ni tukio la pili kutokea eneo hilo la Mkata.
Aliongeza kuwa, tukio la kwanza lilitokea Januari 14 mwaka huu, ambapo mtoto mwenye umri wa miaka nane alibakwa kwa madai ya kutukuza imani za kishirikina wakidai mtoto akifanyiwa kitendo hicho, familia husika itapata pesa nyingi.
Babu wa mtoto (jina linahifadhiwa), anadaiwa kushikiliwa kwenye Kituo cha Polisi Mkata kwa kosa la ubakaji.


    

0 comments: